BUKINA FASO YATIMUA KOCHA MSAIDIZI
SHIRIKISHO
la Soka nchini Burkina Faso limemtimua kocha msaidizi wa timu ya taifa ya nchi
hiyo Sidi Napon baada ya kugombana na kocha mkuu Paul Put. Katika taarifa
yake shirikisho hilo limedai kuwa wameshindwa kuvumilia tabia Napon ya
kutomuheshimu mwenzake na wameamua kumuengua katika timu ya wakubwa na kumpa
timu ya watoto. Meneja wa timu hiyo Gualbert Kabore naye pia alitimuliwa
baada ya kuwatuhumu viongozi kutojumuisha jina lake katika orodha ya watu
waliotunukiwa medali na rais wakiwemo wachezaji mara baada ya kurejea kutoka
katika michuano ya Mataifa ya Afrika iliyofanyika nchini Afrika Kusini.
Shirikisho
hilo sasa limekabidhi majukumu yote Put ambaye ni raia wa Ubelgiji kuhakikisha
timu hiyo inafanikiwa kufuzu kwa mara kwanza michuano ya Kombe la Dunia
itakayofanyika nchini Brazil mwaka 2014 wakati wakitafuta watu wataoziba nafasi
zilizoachwa wazi katika benchi la ufundi.
No comments:
Post a Comment