KOMBE LA CHALLENGE MWAKA HUU KUFANYIKA NAIROBI
NCHINI KENYA.
Kenya Imepata
tikiti ya kuandaa mashindano ya kombe la chalenji.
Shirikisho la
soka la kenya (FKF) limepata haki hiyo katika mkutano wa CAF
uliofanyika huko Marrakech, Morocco.
Ambapo Mechi
zitachewza katika kiwanja cha kimataifa cha Moi na Nyayo huko Nairobi pamoja
na Kisumu Uwanja wa Moi ambao kwa sasa upo kwenye matengenezo
ambao unafadhiliwa katika mradi wa fifa
( FIFA Goal
Project) utakuwa tayari baada ya miezi mitatu .
"Huu ni
wakati mzuri kwetu kwa soka la kenya na tunashukuru kwa msaada wa serikali na
tunaamini tutaandaa mashindano bora zaidi katika ardhi ya kenya
alisema Mwenyekiti wa shirikisho la soka la kenya ," FKF Sam
Nyamweya .
"Vile
vile tumeomba kuaanda michuano ya vilabu bingwa afrika mashariki na kati na
kutakuwa na mkutano wa cecafa kuatazama uwezekano wa jambo hilo .
Kenya
iliandaa mara ya mwisho michuano hiyo mwaka 2009 na mwaka jana
iliandaliwa na Uganda.
No comments:
Post a Comment