BARCELONA YATINGA
ROBO FAINALI KWA KISHINDO YAIBUGIZA AC MILANI 4-0
![]() |
Messi |
Timu ya Barcelona imetinga
hatua ya robo fainali baada ya kuichakaza AC Milan mabao 4-0 na kuitoa nje ya ligi
ya mabingwa mchezo ulipigwa katika dimba la Camp Nou usiku wa kuamkia leo.
Ikiwa na deni la
bao mbili iliweza kusawazisha magoli yote na kufunga mengine mawili na kutoka
na ushindi wa mabao manne kwa sifuri
Goli la kwanza
lilipatikana katika dakika ya tano ya mchezo
na Lionel Messi kwa shuti kali na nje ya
kumi na nane.
Alikuwa Messi tena pale
aliposhindilia goli la pili Dk ya 40 na kuisaidia timu yake kwenda mapumziko wakiwa
mbele kwa mabao 2-0.
David Villa
alifunga bao la tatu dk ya 55 baada ya kutengenezewa pasi maridadi
na Xavi lakini badae Jordi Alba alihitihimisha ushindi katika
dk ya 90 kwa Barca na kutoka na ushindi huo wa mabao 4-0 .
Katika mchezo mwingine timu ya Galatasaray
nayo imeweza kufuzu hatua ya robo fainali baada ya kuitoa nje ya mashindano
timu ya Shalke 04 mabao 3-2.
Mabao ya Gatasaray
yakipachikwa na Altintop
37, Yilmaz 42, Bulut 90+4
Huku mabao ya shalk yakifungwa na Neustadter
17, Michel Bastos 63.
Mbali na Barcelona
na
Galatasaray Timu nyingine ambazo zimeshingia robo
fainali mpaka sasa ni Borussia Dortmund,
Juventus, Paris St Germain na Real Madrid.
Michuano hiyo inaendelea tena leo kwa
mechi kati ya
Bayern Munich dhidi ya Arsenal, huku Malaga wakiwakaribisha Porto.
No comments:
Post a Comment