KIM POLSEN AITA WACHEZAJI 23 KUIKABILI MOROCCO
![]() |
| Kim Polsen |
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ametaja wachezaji 23 watakaoingia
kambini Jumamosi (Machi 16 mwaka huu) jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mechi
ya mashindano dhidi ya Morocco.
Mechi hiyo ya mchujo kuwania tiketi ya
kucheza fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwakani nchini Brazil
itachezwa Machi 24 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Kocha Kim, wachezaji wa Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager wanatakiwa kuripoti kambini katika hoteli ya Tansoma, Machi 17 mwaka huu.
Kwa mujibu wa Kocha Kim, wachezaji wa Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager wanatakiwa kuripoti kambini katika hoteli ya Tansoma, Machi 17 mwaka huu.
Wachezaji walioitwa ni makipa Juma Kaseja
kutoka Simba ambaye pia ndiye nahodha wa Stars, Aishi Manula (Azam), Hussein
Shariff (Mtibwa Sugar) na Mwadini Ally (Azam).
Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Erasto
Nyoni (Azam), Issa Rashid (Mtibwa Sugar), Kelvin Yondani (Yanga), Nadir Haroub
(Yanga), Nassoro Masoud Cholo (Simba) na Shomari Kapombe (Simba).
Viungo ni Salum Abubakar (Azam), Athuman
Idd (Yanga), Amri Kiemba (Simba), Khamis Mcha (Azam), Frank Domayo (Yanga),
Mwinyi Kazimoto (Simba) na Shabani Nditi (Mtibwa Sugar).
Washambuliaji ni John Bocco (Azam), Mbwana
Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Mrisho Ngasa
(Simba), Simon Msuva (Yanga), na Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe, Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Congo (DRC).
Mbali ya Kim, benchi la ufundi la Taifa
Stars linaundwa na Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi), Juma Pondamali (Kocha wa
makipa), Leopold Tasso (Meneja), Dk. Mwanandi Mwankemwa (Daktari wa timu),
Frank Mhonda (Mtaalamu wa tibamaungo) na Alfred Chimela (Mtunza vifaa).

No comments:
Post a Comment