FIFA YAIPA ONYO CONGO DR
SHIRIKISHO
la Soka la Dunia-FIFA limetuma barua rasmi kwa Wizara ya Michezo nchini Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Congo-DRC kuitaka kuondoa tarehe ya kuzitaka klabu zote
nchini humo kucheza mechi zao za ligi katika viwanja vinavyomilikiwa na
serikali. Wakosoaji na wachambuzi wa soka ndani ya nchi hiyo wanaamini
kuwa tamko hilo linailenga klabu ya TP Mazembe ambayo mwaka jana ilifungua
kituo chake binafsi cha michezo.
FIFA
limeitaka wizara hiyo ambayo inaongozwa na Banza Mukalay Nsungu kubadilisha
uamuzi wake au wapewe adhabu ambayo inaweza kuathiri timu ya taifa ya nchi hiyo
pamoja na vilabu vinavyoshiriki michuano iliyoandaliwa na Shrikisho la Soka
barani Afrika-CAF. TP Mazembe ambayo ina maskani yake jijini Lubumbashi
ilizindua uwanja wake mpya Juni mwaka jana ambao una uwezo wa kuchukua
mashabiki 19,500, ukiwa ni mwa mmoja umepita toka wanunue ndege yao wenyewe
yenye uwezo wa kubeba watu 140.
No comments:
Post a Comment