Thursday, March 14, 2013


JAMAA AMUA  KUFUNGA NDOA NA MPENZI WAKE ALIYE KUFA ILI KUTIMIZA AHADI YAKE.
Deffy akimvisha pete Kamsook
Hapa akimpusu mchumba wake marehemu
Mtu mmoja huko nchini Thailand hivi karibuni ameamua kumuoa mpenzi wake aliyekufa lengo ni kutimiza ahadi yao waliyojiwekea ya kuoana siku za usoni.
Chadil Deffy alimvisha pete ya ndoa mchumba wake Anne Kamsook katika siku ya mazishi ambayo pia ilikuwa siku ya sherehe ya harusi hiyo.
Deffy na Kamsook waliwekeana ahadi ya kuoana siku za usoni lakini kwa bahati mbaya Kamsook  alikufa kwa ajali kwa bla ya kutimiza adhima yao ya kuoana.
Deffy alihisi hatakuwa amemtendea vema mchumba wake kutengana bila kufunga ndoa ndipo alipoamua kuchukua maamuzi hayo.
Mbele ya ndugu, jamaa na marafiki  Deffy alimvisha pete mchumba wake marehemu na kuhaidi kumpenda maisha yake yote.
Kamsook alizikwa baada ya sherehe kumalizika.

No comments: