Thursday, March 14, 2013

ARSENAL YAIBANJUA BUYERN 2-0 NYUMBANI LAKINI YASHINDWA KUINGIA ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA

Olivier Giroud akifunga bao la mapema lililowatia presha wenyeji 
Laurent Koscielny akifunga bao la pili kwa kichwa dakika za mwishoni

Wenger akilalamikia uamuzi wa refa
KLABU ya Arsenal imetolewa kiume katika Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wan kuamkia leo baada ya kushinda 2-0 ugenini dhidi ya Bayern Munich nchini Ujerumani.
Matokeo hayo yanamaanisha matokeo ya jumla ni 3-3 baada ya awali, Bayern kushinda 3-1 Jijini London.
Bayern imesonga mbele kwa faida ya mabao ya ugenini na sasa imejikita Robo Fainali.
Olivier Giroud aliifungia Arsenal bao la kwanza dakika ya tatu ambalo lilidumu hadi mapumziko. 
Laurent Koscielny akaja kuwafungia la pili The Gunners dakika ya 86, lakini Bayern wakabebwa na mabao yao ya ugenini kusonga mbele.
katika mchezo mwingine timu ya Malaga imewabamiza Porto mabao 2-0 na kufanikiwa kutinga hatua ya robo fainali. 

No comments: