Wednesday, December 19, 2012

TANZANIA YAPANDA NAFASI NNE KATIKA VIWANGO VYA FIFA
Tanzania imepanda kwa nafasi nne katika viwango vya ubora wa soka duniani vinavyotolewa na shirikisho la soka duniani FIFA kutoka nafasi ya 134 mpaka 130.
Katika viwango hivyo hispania bado ikiongoza, ikifuatiwa na Ujerumani, Argentina inashika nafasi ya tatu, Italy ya nne huku Kolombia ikkamata nafasi ya tano.
Brazil imeporomoka kwa safasi tano kutoka nafasi ya 13 mapaka nafasi ya 18 duniani.
Barani Afrika Ivory coast ndiyo inaongoza ikiwa nafasi ya 14 duniani, ikifuatiwa na  Algeria ikishika nafasi ya 19 duniani wakati Mali inashika nafasi ya 25 duniani, huku Mabingwa wa Afrika Zambia ikikamata nafasi ya 35 duniani

No comments: