Wednesday, December 19, 2012

KIJANA AUAWA HADHARANI KWA KOSA LA KUMBAKA KIKONGWE CHA MIAKA 80
Kijana mmoja Nchini kenya amejikuta akiingia katika matatizo mazito akiwa katikati ya wananchi wenye hasira kali mara baada ya kumbaini kuwa alimlawiti na kumbaka bibi kizee wa miaka 80. 
Tukio hilo liliwafanya watu kukosa uvumilvu wa nafsi na kuamua mkushambulia kijana huyo ambaye juhudi za Polisi kutaka kuunusuru uhai wake uligonga mwamba kwani mwisho wa siku alipoteza maisha mikononi mwa wananchi  hao ambao walionekana kuchoshwa na matendo ya Ubakaji.

Habari kutoka Katika kijiji cha Kichacha kulikotokea tukio hilo, bibi mmoja ambae jina limehifadhiwa alipovamiwa na vijana wawili nyumbani kwake na kumdai Kshs 15,000 na kumfanyia kitendo hicho cha aibu cha Ubakaji.

Kwa bahati nzuri katika  purukushani za hapa na pale bibi huyo alifanikiwa kubonyeza  Alarm ya kuashiria Hatari ndipo vijana hao walipoamua kutimua Mbio.

Lakaini bahati haikuwa yao vijana hao kwani walipojaribu kukimbia walikamatwa na wananchi ambao walisikia makelele ya bibi wakati akibakwa na ndipo walipoanza kuwapigwa kwa mawe na kuwajeruhi vibaya hao na mmoja wao alibahatika kunuriwa na POLISI lakini mwingine alifariki hapo hapo.


No comments: