Thursday, November 20, 2014

FAINALI za Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2015, ambazo zitachezwa kuanzia Januari 17, tayari zimeshapata Washiriki 15 watakaojumuika na Wenyeji Equatorial Guinea baada ya Mechi za mwisho za Makundi hapo Jana.
Kila Kundi limetoa Timu mbili kufanya Jumla ya Timu 14 na ya 15 ni ile iliyomaliza Nafasi ya 3 Bora toka Kundi lake ukilinganisha na nyingine za Nafasi hiyo.
Mabingwa Watetezi Nigeria wameshindwa kufuzu baada ya kutoka Sare 2-2 na South Africa kutoka Kundi A.

Kwa upande wa eneo la Afrika Mashariki kuwa matumaini yameyeyuka baada ya mwakilishi pekee wa eneo hilo timu ya Uganda kucharazwa na Guinea

Uganda iliyokuwa na pointi 7 kama Guinea ilitakiwa kushinda mchezo huo. Ghana inaongoza kundi hilo ikiwa na pointi 11.

Katika kundi hilo Ghana imeicharaza Togo 3-1. Timu za Uganda na Togo zimeaga michuano hiyo.

Mabingwa wa zamani wa michuano hiyo kwa mwaka 1968 na 1974, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo(Zaire), imefanikiwa kutinga katika michuano ya mataifa ya Afrika mwakani kwa kuwa na wingi wa pointi kati ya timu zote zilizoshika nafasi ya tatu katika makundi yote nane.

Timu ya DR Congo waliofuzu kucheza fainali za Caf za 2015 baada ya kuwa timu bora iliyoshika nafasi ya tatu ikilinganishwa na timu za nafasi hiyo za makundi mengine

DR Congo imeibuka na pointi 9.

Timu zilizofuzu kutoka kila kundi ni kama ifuatavyo:

Kundi A: Afrika Kusini yenye pointi 12 na Congo pointi 10. Nigeria na Sudan zimetupwa nje.

Kundi B: Algeria na Mali zimesonga mbele kwa alama 15 na 9 kama zinavyofuatana, huku Angola na Lesotho zikifungasha virago.

Kundi C: Gabon na Burkina Faso zimetinga hatua ya fainali kwa kujikusanyia alama 12 na 11 kama zinavyofuatana.

Kundi D: Cameroon, Ivory Coast na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo zina pointi 14, 10 na 9 kama zilivyoongozana. Sierra Leone imetupwa nje.

Kundi E: Ghana na Guinea kwa alama 11 na 10. Uganda na Togo zimeyaaga mashindano hayo.

Timu ya Misri moja ya vigogo wa soka barani Afrika haitashiriki fainali za Caf 2015 baada ya kushindwa kufuzu katika kundi lake

Kundi F: Cape Verde na Zambia zenye pointi 12 na 11 zikiziacha timu za Msumbiji na Niger.

Kundi G: Senegal na Tunisia zina pointi 13 na 14. Misri na Botswana zimeshindwa kufuzu, pale zilipoambulia pointi 6 na 1 kama zinavyofuatana.

Fainali hizi za Kombe la Mataifa ya Afrika zinafanyika nchini Equatorial Guinea ambayo nayo imepewa nafasi kutokana na kuwa nchi mwenyeji wa michuano, baada ya Morocco iliyokuwa imepewa nafasi ya kuandaa kutaka michuano hiyo kuahirishwa kwa hofu ya ugonjwa wa Ebola ambao umeziathiri nchi za Afrika Magharibi, hususan Liberia, Sierra Leone na Guinea. Vigogo wa soka barani Afrika, Nigeria na Misri hazitaonekana katika fainali hizo.

No comments: