WANAFUNZI CHUO KIKUU ZIMBABWEW WAPINGA SHERIA INAYOZUIA ‘KUPIGANA MABUSU
Muungano
wa wanafunzi umelaani sheria mpya iliyopitishwa na chuo kikuu cha Zimbabwe
ambayo inapiga marufuku wanafunzi hao ‘kupigana mabusu’.
Taarifa
iliyoandikwa na shirika la utangazaji Uingereza BBC, imesema kiongozi wa
muungano wa wanafunzi Zimbabwe, Gilbert Mutubuki amesema wataungana kuipinga
sheria hiyo kandamizi inayowanyima uhuru na kuwafanya wanafunzi hao wa chuo
kikuu kulinganishwa na watoto wa chekechea.
Katika
vipeperushi vilivyobandikwa sehemu mbali mbali chuoni hapo, vimeandikwa amri
kuwa yoyote atakayekutwa katika mazingira ya kutatanisha kama vile kupigana
mabusu ama kufanya mapenzi hadharani ataadhibiwa vikali.
Vile
vile sheria hiyo imekataza wanafunzi kuwaingiza wenzao wa jinsia tofauti katika
mabweni yao, pamoja na kuleta marafiki zao katika eneo la chuo ambapo wamesema
ni sheria inayowanyima haki ya kujumuika na wenzao.
Wanafunzi
wa vyuo vikuu nchini humo wamekuwa wakipingana na serikali mara kwa mara,
ambapo kwa sasa kiongozi huyo wa wanafunzi amehimiza wanafunzi wenzake kuipinga
sheria hiyo.
No comments:
Post a Comment