BWANA HARUSI AFARIKI AKIENDA HARUSIN
Takriban
watu 17 akiwemo bwana harusi na watoto wawili wamekufa maji baada ya boti ya
uokoaji iliyokuwa imewabeba wageni kwenda kwa sherehe ya harusi kuzama katika
mafuriko nchini Pakistan.
Maafisa
wanasema kuwa takriban watu 22 wameokolewa huku waokoaji wakiwatafuta watu
zaidi.
Msemaji
wa shirika la kukabiliana na majanga amesema kuwa zaidi ya watu millioni 2
nchini humo waliathiriwa na mafuriko hayo ambayo yalisababishwa na mvua kubwa.
Maafisa
wanasema kuwa takriban watu 289 wamefariki katika mafuriko hayo nchini Pakistan
kufikia sasa.
Zahid
Ali mwenye umri wa miaka 27,mchumba wake Mashal pamoja na wageni walikuwa
katika boti hiyo iliyokuwa ikielekea katika sherehe za kundeleza harusi yao.
Watu
18 waliokuwa wanakwenda kushuhudia harusi wameaga dunia
Maafisa
wanasema kuwa boti hiyo iliojaa kupitia kiasi ilikuwa ikivuka mto Chenab
uliofurika katikati ya mji wa Punjab eneo lililoathirika vibaya na mafuriko
nchini Pakistan.
Msemaji
wa huduma ya uokozi katika eneo hilo la Punjab amesema kuwa familia hiyo ilionywa
kuhusu mafuriko hayo.
Bi
harusi amesema kuwa alinusurika baada ya kushika mti wa stima.
Mazishi
ya waathiriwa 17 yamefanyika huku waokoaji wakiendelea kuwatufuta wale
waliotoweka.
BBC
BBC
No comments:
Post a Comment