Friday, September 12, 2014

OSCAR HATIANI KWA KUUA BILA KUKUSUDIA

Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius, amepatikana na hatia ya kumuua mpenziwe Reeva Steenkamp kwa bahati mbaya
Akitoa uamuzi wake jaji Thokozile Masipaal alisema kuwa mwanariadha huyo alimuua Reeva kwa bahati mbaya alipofyatua risasi kupitia kwa mlango wake wa choo akiw akatika hali ua mshtuko akidhani kuwa jambazo alikuwa amevamia nyumba yake.
Alisema kuwa upande wa mashitaka umeshindwa kuthibitisha kuwa Pistorius alinuia kumuua Steenkamp nw akutekeleza mauaji hayo kwa kusudi.
Pia alipatikana na hatia ya kosa la kutumia silaha yake visivyo alipokwenda mgahawani
BBC Swahili.

No comments: