KIUNGO mahiri wa klabu ya Arsenal Jack Wilshere amekiri
na kujutia kitendo chake cha kuvuta sigara katika picha aliyopigwa akiwa katika
likizo ya Kombe la Dunia na kusisitiza kuwa atafanya jitihada kuhakikisha
anarejea katika kiwango chake bora msimu huu unaokuja. Wilshere alizua
utata wakati picha ikimuonyesha akivuta sigara katika bwawa la kuogolea jijini
Las Vegas ilipovuja mapema mwezi huu, muda mfupi baada ya Uingereza kutolewa
katika michuano ya Kombe la Dunia. Meneja Arsene Wenger amekuwa akiipinga
vikali tabia hiyo kwa wachezaji wake na toka wakati huo amefanya nae mazungumzo
na nyota huyo mwenye umri wa miaka 22 amekiri hadharani kuwa alifanya tukio
hilo na kwamba ni bahati mbaya. Akihojiwa Wilshere amesema anajutia
kitendo chake hicho hususani kwa kukirudia kwa mara ya pili na kudai kuwa bado
ana umri mdogo hivyo anajifunza kutokana na makosa anayofanya.
No comments:
Post a Comment