Thursday, April 24, 2014

BAO la Dakika ya 19 la Karim Benzema limewapa Real Madrid ushindi wa Bao 1-0 dhidi ya Mabingwa Watetezi Bayern Munich kwenye Mechi ya Kwanza ya Nusu Fainali ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI iliyochezwa Uwanja wa Santiago Bernabeu huko Madrid, Spain usiku wa kuamkia leo.

Timu hizi zitarudiana huko Allianz Arena, Jijini Munich Jumanne Aprili 29.

Wakati Bayern wanawania kuwa Timu ya Kwanza kufanikiwa kutetea Taji lao, Real wanataka kufuta uteja toka Bayern ambayo imeitoa katika Nusu Fainali 4 kati ya 5 walizokutana kwenye Mashindano haya ya Ulaya.

Jumanne Usiku, kwenye Mechi nyingine ya Kwanza ya Nusu Fainali iliyochezwa huko Estadio Vicente Calderon Jijini Madrid, Atletico Madrid na Chelsea zilitoka Sare ya 0-0.

Marudiano

Jumanne Aprili 29

Bayern Munich v Real Madrid [0-1]

Jumatano Aprili 30

Chelsea v Atletico Madrid [0-0]

FAINALI:

Estádio da Luz, Lisbon, Portugal 24 Mei 2014

Bayern Munich/Real Madrid v Chelsea/Atletico Madrid

No comments: