Thursday, April 10, 2014

AZAM YANYEMELEA UBINGWA 
AZAM FC sasa inahitaji pointi 3 kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom baada ya leo huko Mabatini, Mlandizi kuichapa Ruvu Shooting Bao 3-0.
Mechi hii ilikuwa ichezwe Jana lakini ikaahirishwa kutokana na Mvua kubwa.
Wakiwa wamebakisha Mechi mbili, ile na Mbeya City huko Mbeya na JKT Ruvu Uwanja wa Azam Complex, Azam FC wanahitaji Pointi 3 tu kutwaa Ubingwa bila ya kujali nini Timu ya Pili, Yanga, ambao ndio Mabingwa Watetezi, wanakifanya nini.
Hivi sasa Azam FC wanaongoza Ligi wakiwa na Pointi 56 na kufuatiwa na Yanga wenye Pointi 52 na ambao wamebakisha Mechi mbili dhidi ya JKT Oljoro, huko Arusha, na Simba.
Bao za Azam FC  Leo hii  zilifungwa na Gaudence Mwaikimba, Himid Mao na Kipre Tchetche.
Mechi inayofuata kwa Azam FC ni hapo Jumapili watakapokuwa Mbeya kucheza na Mbeya City na Siku hiyo hiyo Yanga watakuwa Arusha kuivaa JKT Oljoro.
RATIBA:
Jumamosi Aprili 12
Mtibwa Sugar vs Ruvu Shooting (Manungu, Morogoro),
Coastal Union vs JKT Ruvu (Mkwakwani, Tanga),
Tanzania Prisons vs Rhino Rangers (Sokoine, Mbeya).
Jumapili Aprili 13
Mgambo Shooting vs Kagera Sugar (Mkwakwani, Tanga),
Simba vs Ashanti United (Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam)
Mbeya City vs Azam (Sokoine, Mbeya)
JKT Oljoro vs Yanga (Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha).


MSIMAMO:
NA
TIMU
P
W
D
L
GD
GF
PTS
1
Azam FC
24
16
8
0
34
48
56
2
Yanga SC
24
15
7
2
41
58
52
3
Mbeya City
24
12
10
2
13
30
46
4
Simba SC
24
9
10
5
15
40
37
5
Kagera Sugar
25
8
11
6
2
22
35
6
Ruvu Shooting
24
9
8
7
-3
27
35
7
Mtibwa Sugar
25
7
10
8
0
28
31
8
Coastal Union
24
6
11
7
-2
16
29
9
JKT Ruvu
23
8
1
14
-19
19
25
10
Mgambo Shooting
23
6
6
11
-16
16
24
11
Ashanti UTD
23
4
7
12
-20
17
19
12
JKT Oljoro
24
3
9
12
-17
17
18
13
Prisons FC
22
3
9
10
-11
17
18
14
Rhino Rangers
23
3
7
13
-17
15
16

No comments: