RAGE AWATANGAZA EZEKIEL KAMWAGA KUWA KATIBU SIMBA, ASHA MUHAJI AFISA HABARI MPYA.
KLABU ya Soka ya Simba imefanya mabadiliko ya
sekretarieti yake pamoja na kutangaza tarehe ya kufanya Mkutano Mkuu
maalumu. Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa klabu hiyo Ismail
Aden Rage amesema wamefikia hatua hiyo baada ya kufanyika kwa kikao cha Kamati
ya Utendaji.
Rage amesema nafasi ya Katibu Mkuu wa klabu sasa
itashikiliwa na aliyekuwa ofisa habari wake Ezekiel Kamwaga akisaidiwa na
Stanley Philipo, nafasi ya muhasibu ikibakia kwa Eric Sekiete akisaidiwa na
Amina Kimwambi.
Nafasi ya ofisa habari sasa itashikiliwa na Asha Muhaji
huku meneja wa timu akiwa Hussein Mbozi na Issa Mathayo atakuwa
msimamizi.
Rage pia amesema katika kikao hicho wamepanga Machi 23
mwaka huu kuwa tarehe ya Mkutano Mkuu Maalumu ambao utakuwa na ajenda moja ya
kuhusu mabadiliko ya katiba.
Wakati huohuo Rage amesema wamepokea barua kutoka kwa
Mwanasheria Mkuu wa Kamati ya Hadhi za Wachezaji wa Shirikisho la Soka Duniani,
FIFA ambayo inawataka klabu ya Etoul du Sahel hadi Januari 27 mwaka huu wawe
wametoa maelezo kuhusiana na hela ya mshambuliaji Emmanuel Okwi.

No comments:
Post a Comment