![]() |
| Thomas Chirembwe |
MAHAKAMA
moja ya Zimbabwe imemfunga jela miaka 290 mwanamume mwenye mazoea ya kuwabaka
wanawake.
Thomas Chirembwe anasemekana kuwadhulumu kimapenzi takriban wanawake 13.
Chirembwe, 30, alipatikana na makosa 21 ya ubakaji na ujambazi baada ya muda mrefu wa kuendeleza uhalifu katika mji mkuu Harare.
Akitoa adhabu hiyo, Hakimu Simon Rogers Kachambwa alimtaja Chirembwe kama “mwovu zaidi ya mnyama wa mwituni” kwa

sababu
aliwabaka wanawake kwa 'kujifurahisha’.
Miaka 60 ya kifungo hicho yaliwekwa kando kwa sharti kwamba atabadilisha tabia, na kumwacha na miaka 230 jela.
Chirembwe alikuwa akikabiliwa na makosa 30 ya ubakaji na kuingia pahali bila ruhusu lakini kesi tisa hazikusikizwa baada ya mashahidi kukosa kufika kortini.
Korti iliambiwa kuwa alitumia silaha kama vile visu, chuma na spana kuwatisha wahasiriwa kabla kuwabaka.
“Katika vitendo vyake vya uhalifu, pia aliwabaka wanawake na kuiba pesa na bidhaa zingine za thamani,” hakimu kasema: “Hakuna tashwishi yoyote kwamba alikuwa amegeuza uhalifu kuwa taaluma, aliyotumia kujikimu maisha.
Waendesha mashtaka walimtaja Chirembwe kama “gaidi wa mjini wa pekee” aliyevunja nyumba za watu na kuwabaka wanawake 13 kati ya Septemba 18, 2011 na Novemba 6, 2012.
Pia aliiba mali ya thamani ya maelfu ya dola na pesa taslimu baada ya kuwabaka wanawake hao bila kutumia kinga.

http://nehandaradio.com

No comments:
Post a Comment