Wednesday, January 29, 2014

MENEJA wa Hull City, Steve Bruce, anataka Marefa wa Ligi Kuu England nao wazikabili Kamera za Wanahabari mara baada ya Mechi wahojiwe na ametoa msimamo wake huo Jana mara baada ya Timu yake kufungwa 1-0 na Crystal Palace kwenye Mechi ya Ligi, kunyimwa Penati mbili na mwishowe Kipa wao kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu.
Katika Mechi hiyo Jason Puncheon ndie aleifunga Bao pekeke liloifanya Palace ifungane kwa Pointi na Hull.
Lakini Sekunde 90 tu baada ya Puncheon kufunga Bao hilo, Straika wa Hull Shane Long aliangushwa kwenye Boksi na Refa Roger East akapeta tu.
Steve Bruce alifoka: “Kuna maamuzi mabovu matatu dhidi yetu na ambayo yametufanya tufungwe. Nadhani Marefa wanapaswa kuhojiwa baada ya Mechi mbele ya Kamera!”
Tukio jingine ni pale Mchezaji wa Hull Nikica Jelavic alipoangushwa na Refa East pia kufumba macho.
Bruce aliongeza: “Hii inasikitisha. Wiki mbili zilizopita nilipigwa Faini kuhusu maoni yangu juu ya Marefa na sitaki kurudia tena. Lakini zile ni Penati za wazi na kumtoa Kipa wetu kwa kosa dogo ni kitu ajabu. Mie nalipa Faini, na Faini, na pengine nitalipa tena. Wao waletwe mbele ya Kamera na kuulizwa Maswali! Wanalipwa vizuri kutoa maamuzi makubwa lakini Leo hakufanya hivyo!”

No comments: