Friday, January 10, 2014


Mkazi wa mmoja wa kijiji cha Nang’ondo, Wilaya ya Nachingwea, mkoani Lindi anashikiliwa na jeshi la polisi baada ya kumuua baba yake mzazi katika harakati ya kumwokoa shangazi yake aliye alikuwa anabakwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, George Mwakajinga, alisema tukio hilo limetokea siku ya mkesha wa mwaka mpya saa 4 usiku ambapo Bw. James Leslie (20) akiwa njiani kuelekea nyumbani alisikia kilio cha mtu kichakani kando ya njia akiomba
msaada na aliposogea akakuta baba yake, Leslie Amuri (45) akimbaka huku amemkaba shingoni dada yake Esha Amuri (68).

Mwakanjinga alisema, James alijaribu kumtoa mikono baba yake ili asiendelee kumkaba shagazi yake lakini hakufanikiwa,  akihofia maisha ya shangazi yake, alianza kumpiga baba yake  mikononi ili amuachie lakini kutokana na giza akampiga kichwani na ndipo alipofariki kwenye eneo la tukio.

“Mtuhumiwa alikuwa anatoka kwenye sherehe za mwaka mpya usiku na ndipo aliposikia sauti ya mtu akigumia kichakani kando ya njia aliyokuwa anapitia na ndipo kwa lengo la kumwokoa shangazi yake alijaribu kumgandua baba yake lakini alishindwa hivyo akalazimika kutumia magongo ambayo alimpiga kichwani na kumsababishia maumivu makali na kumuua baba yake papo hapo,”alisema Mwakanjinga.

Kamanda huyo alisema jeshi la polisi linamshikilia mtuhumiwa James Leslie na kuwa linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.
Majira

No comments: