ACHINJA MPENZI WAKE KWA KUMTUHUMU NI MALAYA KISHA
AJIUA
![]() |
Kamanda wa Polisi wa Mkoa Iringa, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Ramadhan Mungi |
Kamanda wa Polisi wa Mkoa Iringa, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Ramadhan Mungi, alisema mauaji hayo yamesababishwa na wivu wa mapenzi.
“Mauaji yametokea Desemba 27, ambapo mwanaume huyo alimchinja mpenzi wake Anna Mpinga (30) na kutenganisha koromeo na kiwiliwili, na kisha kumfunika na blanketi kitandani,” alisema.
Alisema kuwa mwanaume huyo alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanamke aliyemchinja kwa muda baada ya kuachika kwa mumewe, lakini mahusiano yao yalitawaliwa na ugomvi wa mara kwa mara.
Kwa mujibu wa Kamanda Mungi, mara kwa mara mwanaume huyo alikuwa akimtuhumu mpenzi wake kutokuwa mwaminifu kipindi cha uhusiano wao.
Alifafanua kuwa siku ya tukio hilo, wakiwa chumbani kabla ya kujiua kwa sumu, alimchinja mpenzi wake kwa kumpitishia kisu shingoni na kukata koromeo na kuhamia sehemu ya kinywa ambapo alimkata sehemu ya mdomoni hadi usawa wa taya.
Aliongeza kuwa mara baada ya kumaliza unyama huo, aliufunika mwili wa marehemu na kuacha ujumbe uliosomeka; “Nimemchinja mwenyewe nimemwambia aache umalaya.”
Kamanda alisema kuwa mwanaume huyo akiwa mtaani alikunywa pombe aina ya Vodka kisha kunywa sumu na kujiua.
Alisema kuwa miili yote iligunduliwa na majirani na baadaye kutoa taarifa polisi ambapo baada ya uchunguzi ilizikwa kijijini hapo huku upelelezi ukiendelea.
Tanzania daima
No comments:
Post a Comment