AYA TOURE ATWAA TUZO YA MWANASOKA BORA ZAIDI AFRIKA
Mchezaji huyo wa Ivory Coast, na ambaye pia
ni kiungo wa klabu ya Manchester City ya Uingereza, na ambaye jina lake
limekuwepo kwa miaka minne iliyopita katika orodha ya wachezaji wanaowania
tuzo, aliwashinda Pierre-Emerick Aubameyang, Victor Moses, John Mikel Obi na
Jonathan Pitroipa, katika kuibuka mshindi.
Orodha fupi ya waliowania tuzo hiyo
ilitayarishwa na wataalamu 44 wa soka kutoka kote barani Afrika, na
wakizingatia hasa maarifa ya mchezaji, kiufundi, ushirikiano na wenzake katika
timu, na kwa kucheza mchezo safi na kwa haki.
Kisha, kupitia idadi kubwa kabisa
kuandikishwa kwa wapiga kura, mashabiki waliweza kushiriki katika shughuli hiyo
katika mtandao, au kupitia ujumbe wa simu ya mkononi.
Mashabiki hao wameamua kwamba Toure ndiye
bora zaidi, kwani katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, raia huyo wa Ivory
Coast alicheza kwa bidii, kuonyesha mchezo wa kasi, ubunifu, na vile vile kwa
kufunga magoli.
Ingawa mwaka 2013 ulikuwa ni wa ufanisi kwa
Toure hasa kwa kupata vikombe, hakuweza kuisaidia nchi yake, wala klabu, kupata
kombe lolote lile, lakini bado alionyesha kiwango cha hali ya juu katika
mchezo.
Baada ya kuvunjika moyo kwa kushindwa
kuutetea ubingwa wao wa ligi kuu ya Premier wa mwaka 2012 akiichezea Manchester
City, Toure alirudi uwanjani akijizatiti, na kuimarisha mikwaju yake ya free-kick.
Alitumbukiza wavuni bao, kwa mpira wa
kupinda, katika siku ya kwanza ya msimu mpya wa ligi kuu ya Premier, wakati
timu yake ilipocheza na Newcastle, na akarudia hayo hayo katika mechi
iliyofuata wakati Hull walipowatembelea katika uwanja wao wa nyumbani.
Toure amefunga magoli manne ya kupanga kwa
makini shambulio, na hayo yakiwa ni kati ya magoli saba kwa jumla aliyoweza
kuifungia klabu ya Man City msimu huu.
Kufikia sasa, mwaka huu wa 2013, Toure
ametumbukiza wavuni jumla ya magoli 12; ya klabu na vile vile ya nchi yake, na
hiyo ni rekodi nzuri sana kwa mchezaji wa kiungo cha kati.
Mbali na ustadi huo katika kumalizia, Toure
ni kiongozi bora katika timu, na maarifa yake yameiwezesha City kufikia sasa
kuwa katika nafasi ya nne katika ligi kuu ya England.
Aliisaidia kikamilifu nchi yake ya Ivory
Coast kufuzu kwa michuano ya Kombe la Dunia ya mwaka ujao itakayofanyika nchini
Brazil.
Timu yake ya Tembo, The Elephants
ilihitaji kuusahau mwanzo mbovu hapo awali katika kampeni yao ya michuano ya
Kombe la Mataifa ya Afrika, na walipoondolewa katika robo fainali na Nigeria,
ambao hatimaye waliibuka mabingwa, na Toure akiwapa matumaini ya kufanya vyema
baadaye.
Nje ya uwanja, Toure ameongoza vita dhidi
ya ubaguzi wa rangi katika soka, hasa baada ya matusi kuelekezwa kwake katika
mechi ya ligi ya klabu bingwa dhidi ya CSKA Moscow, mwezi Oktoba, na akionyesha
moyo wa uvumilivu na wa kimichezo unaostahili uwanjani.
Tukio kama hilo linaweza kumvunja moyo
mchezaji asiyejiamini, lakini Toure ameendelea kuwa mchezaji wa kipekee tangu
wakati huo.
Na katika mwaka wa tano baada ya jina lake
kupangwa katika orodha ya wachezaji wanaowania tuzo, hatimaye Toure ametajwa
kama mshindi wa tuzo ya mchezaji bora zaidi wa soka barani Afrika.
BBC
No comments:
Post a Comment