YALIYOJIRI TFF LEO
RUFANI KAMATI YA MAADILI MWISHO OKT 2
Wakati walalamikiwa waliofikishwa kwenye Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wakiwa wameshapokea uamuzi dhidi yao kwa maandishi, mwisho wa kukata rufani Kamati ya Rufani ya Maadili ni kesho (Oktoba 2 mwaka huu). Walalamikiwa wote saba waliohudhuriwa mashauli dhidi yao; Kamwanga Tambwe, Nazarius Kilungeja, Omar Abdulkadir, Richard Rukambura, Riziki Majala, Shaffih Dauda na Wilfred Kidao wamepokea uamuzi wa Kamati hiyo inayoongozwa na Jessie Mnguto. Kwa mujibu wa Kanuni za Maadili, kwa ambao hawakuridhika na uamuzi huo wanatakiwa kukata rufani Kamati ya Rufani ya Maadili inayoongozwa na Jaji Mstaafu Stephen Ihema ndani ya siku tatu zinazomalizika kesho. Rufani ziwasilishwe kwa Katibu Mkuu wa TFF kabla ya saa 10 kamili jioni. Kwa mujibu wa Kanuni ya 74 (1) na (2) ya Kanuni za Maadili, rufani zikionesha sababu za kufanya hivyo zinatakiwa kuwasilishwa ndani ya siku tatu kwa njia ya posta (registered post or dispatch or courier service) kwa Sekretarieti. Vilevile inatakiwa rufani inatakiwa kuambatanishwa risiti ya malipo ya ada ya rufani. Ada ya rufani ni sh. milioni moja.
MECHI ZA YANGA, SIMBA ZAINGIZA MIL 182/-

Mechi za Yanga na Simba za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL)
zilizochezwa wikiendi iliyopita jijini Dar es Salaam zimeingiza jumla ya sh.
182,103,000. Yanga katika mechi yake dhidi ya Ruvu Shooting iliyochezwa
Jumamosi (Septemba 28 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kuibuka na
ushindi wa bao 1-0 imeingiza sh. 94,202,000. Watazamaji 16,492 walikata
tiketi kushuhudia pambano hilo ambapo kila klabu ilipata mgawo wa sh.
22,630,921.58. Viingilio katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh.
15,000 na sh. 20,000, na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh.
14,369,796.61. Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh.
11,507,248.26, tiketi sh. 3,117,215, gharama za mechi sh. 6,904,348.96, Kamati
ya Ligi sh. 6,904,348.96, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh.
3,452,174.48 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh.
2,685,024.59. Nayo Simba ambayo iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya
JKT Ruvu katika mechi iliyochezwa Jumapili (Septemba 29 mwaka huu) katika
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 87,901,000. Watazamaji waliokata
tiketi kushuhudia pambano hilo namba 41 walikuwa 15,780. Viingilio katika mechi
hiyo vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu
ikipata mgawo wa sh. 21,051,025.92 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT)
iliyolipwa ni sh. 13,408,627.12. Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia
15 ya uwanja sh. 10,703,911.48, tiketi sh. 3,132,963, gharama za mechi sh.
6,422,346.89, Kamati ya Ligi sh. 6,422,346.89, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa
Miguu (FDF) sh. 3,211,173.44, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam
(DRFA) sh. 1,248,789.67 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA) sh.
1,248,789.67. Wakati huo huo, mechi ya ligi hiyo kati ya Mbeya City na
Coastal Union iliyochezwa Jumamosi (Septemba 28 mwaka huu) Uwanja wa Kumbukumbu
ya Sokoine jijini Mbeya imeingiza sh. 16,959,000 huku kila klabu ikipata sh.
4,035,229. Mgawo wa mechi hiyo ulikuwa ifuatavyo; Kodi ya Ongezeko la
Thamani (VAT) sh. 2,586,966, uwanja sh. 2,051,811.57, tiketi sh. 696,290,
gharama za mechi sh. 1,231,086, Kamati ya Ligi sh. 1,231,086, Mfuko wa
Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 615,543, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa
Mbeya (MREFA) sh. 478,756.
MICHUANO YA CHALENJI KUANZA NOV 27
MICHUANO YA CHALENJI KUANZA NOV 27
Michuano ya Kombe la Chalenji inayoandaliwa na Baraza
la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) inafanyika Kenya
kuanzia Novemba 27 hadi Desemba 12 mwaka huu. Nchi wanachama ambazo
zinataka kushiriki zinatakiwa kuthibitisha ushiriki wao kwa Sekretarieti ya
CECAFA kabla ya Oktoba 20 mwaka huu. Wanachama wa CECAFA ni Burundi, Djibouti,
Eritrea, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Somalia, Sudan, Sudan Kusini, Tanzania,
Uganda na Zanzibar. Michuano hiyo itatanguliwa na Mkutano Mkuu wa CECAFA
utakaofanyika Novemba 26 mwaka huu ambao pamoja na mambo mengine utakuwa na
ajenda ya uchaguzi. Uchaguzi huo ni kwa ajili ya kujaza nafasi nne za wajumbe
wa Kamati ya Utendaji. Wajumbe wanaomaliza muda wao ni Sahilu Gebremarian
wa Ethiopia ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CECAFA, Abdigaani Saed Arab
(Somalia), Tariq Atta (Sudan) na Raoul Gisanura (Rwanda). Majina ya
wagombea yanatakiwa kuwa yamewasilishwa katika Sekretarieti ya CECAFA kabla ya
Oktoba 20 mwaka huu, na yakiwa yamethibitishwa na vyama vyao vya mpira wa
miguu.
SUALA LA PAPIC, YANGA LASUBIRI UAMUZI WA FIFA
SUALA LA PAPIC, YANGA LASUBIRI UAMUZI WA FIFA
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA)
limewasilisha rasmi suala la madai ya aliyekuwa Kocha wa Yanga, Kostadin Papic
dhidi ya klabu hiyo katika Kamati ya Hadhi ya Wachezaji. FIFA imesema
imepeleka rasmi suala hilo katika kamati yake hiyo baada ya kupokea vielelezo
vya Papic anayedai kuidai Yanga dola 10,000 za Marekani pamoja na vile vya
Yanga inayodai kumlipa kocha huyo fedha zote alizokuwa akiidai klabu
hiyo. Kwa taratibu za FIFA, hivi sasa haitapokea vielelezo vingine kutoka
pande hizo mbili, na badala yake Kamati hiyo inayoongozwa na Theo Zwanziger
kutoka Ujerumani itafanya uamuzi na kuziarifu pande husika. Zwanziger kitaaluma
ni mwanasheria. Papic aliyeinoa Yanga kwa vipindi viwili tofauti
aliwasilisha malalamiko yake FIFA akidai hadi mkataba wake unamalizika klabu hiyo
ilikuwa haijamlipa dola 10,000 za Marekani.
LIPULI, MAJIMAJI KUUMANA WAMBI FDL
Mechi ya Ligi Daraja la
Kwanza (FDL) kati ya Lipuli ya Iringa na Majimaji ya Songea sasa itachezwa
kesho (Oktoba 2 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Wambi uliopo Mafinga badala ya
Uwanja wa Kumbukumbu ya Samora mjini Iringa. Mabadiliko hayo yamefanyika
kutokana na Serikali kuutumia Uwanja wa Kumbukumbu ya Samora kwa ajili ya
shughuli za mbio za Mwenge. Mechi nyingine ya FDL kesho itakuwa kati ya
Tessema FC ya Dar es Salaam na Ndanda FC ya Mtwara, na itafanyika kwenye Uwanja
wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam.
LIPULI, MAJIMAJI KUUMANA WAMBI FDL
No comments:
Post a Comment