WABUNGE WANAWAKE WATAKA KATIBA IPIGE MARAFUKU NDOA ZA WATOTO
![]() | |
Angelah Kairuki Naibu Waziri wa Katiba na Sheria |
Akichambua mapendekezo ya rasimu ya Katiba ya Baraza la Katiba la kitaasisi la umoja wa wabunge hao, jijini Dar es Salaam jana, katibu wa umoja huo, Angelah Kairuki, alisema kufanya hivyo kutasaidia kubatilisha ndoa za utotoni.
Kairuki ambaye pia ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria alisema vitendo vya watoto kuolewa katika umri mdogo vimekithiri na vina athari kubwa hapo baadaye, hivyo ni vema suala hilo likapewa kipaumbele.
Wabunge hao pia walitoa mapendekezo yao 50 yakiwa na maoni mbalimbali ikiwa ni pamoja na haki ya mtoto kupewa jina la uraia, kutoa mawazo, kusikilizwa na kulindwa dhidi ya uonevu, ukatili na udhalilishaji.
Alisema ibara ya 56 (2) inatoa haki ya uraia wa kuandikishwa kwa mgeni aliyefunga ndoa na raia wa Tanzania kutokana na kifungu hicho walitoa maoni kuwa raia wa kigeni aombe uraia na kutambulika endapo ndoa hiyo itakaa kwa miaka 10 na baada ya mwanandoa mwenzake kuthibitisha hali ya ndoa yao.
Alisema hiyo itasaidia kuzuia matumizi mabaya ya ndoa ili kupata uraia na kisha kuwatelekeza wanandoa wa Kitanzania.
Tanzania Daima
No comments:
Post a Comment