MTU ANAYESADIKIWA KUWA MREFU ZAIDI KULIKO WOTE DUNIANI HATIMAYE AFUNGA PINGU ZA MAISHA
![]() |
Sultan Kosen mtu mrefu zaidi duniani |
![]() |
Sultan Kosen akiwa na mkewe Mervi Dibo |
Mtu mrefu zaidi duniani Sultan Kosen, Raia wa
Uturuki mwenye urefu wa mita 2.51 (sawa na futi 8.3) amefunga ndoa na mwanamke wa Syria anayemwita
'mpenzi wa maisha yangu', licha ya kumzidi mkewe huyo mita 1.75.
"Siwezi kuelezea hisia zangu kwenye maneno," alisema mume huyo mwenye miaka 31 wakati wa sherehe za harusi hiyo mahali alikozaliwa jimbo la kusini mashariki mwa Mardin Jumapili iliyopita.
"Mimi ni mtu mwenye furaha zaidi duniani," alinukuliwa wakati akisema kwenye tovuti inayoendeshwa na shirika la habari la serikali la Anatolia.
Mkewe mwenye miaka 20, Mervi Dibo, ambaye anatokea kwenye mji wa Syria wa Hasaka, aliongeza: "Natumaini furaha hii itadumu kwa muda mrefu."
Suti ya bwana harusi ilishonwa kwa oda maalumu, ikihitaji mita sita za kitambaa, imeripoti Anatolia.
Akiwa amezaliwa katika familia ya wakulima kusini-mashariki mwa Uturuki, Kosen alishinda tuzo ya mtu maarufu duniani Septemba 2009 pale Guinness World Records ilipomtangaza kuwa mtu mrefu zaidi duniani. Wakati huo alikuwa na urefu wa mita 2.47.
Kosen analazimika kutumia magongo ili aweze kutembea.

No comments:
Post a Comment