TAARIFA MBALIMBALI KUTOKA FIFA
FIFA YAMFUNGIA ABOURAZZOUK WA MOROCCO BAADA YA KUKUTWA MAETUMIA MADAWA KATIKA MCHEZO DHIDI YA TANZANIA.
SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limemfungia miezi sita
mshambuliaji wa kimataifa wa Morocco Hamza Abourazzouk baada ya kukutwa na
chembechembe za dawa za kusisimua misuli katika damu yake.
Abourazzouk mwenye umri wa miaka 27 alikutwa ametumia
dawa hizo katika vipimo aivyofanyiwa baada ya mchezo wa kufuzu michuano ya
Kombe la Dunia dhidi ya Tanzania Juni 8 mwaka huu. Hata hivyo Morocco
walishindwa kufuzu katika michuano hiyo. Nyota huyo anayecheza katika
klabu ya Raja Casablanca atakosa michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia Desemba
mwaka huu ambayo Morocco itakuwa mwenyeji ambapo Raja Casablanca wamefuzu
kushiriki michuano hiyo kama mabingwa wa ligi wan chi hiyo.
WAJERUMANI WAPATA TENDA NA FIFA YA KUFUNGA GOAL-LINE SYSTEM KWENYE KOMBE LA DUNIA BRAZIL.
SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limebainisha kuwa
kampuni ya GoalControl ya Ujerumani ndio itakayofunga kamera za mfumo wa
teknologia ya kompyuta katika goli katika michuano ya Kombe la Dunia 2014
nchini Brazil na Kombe la Klabu Bingwa ya Dunia itakayofanyika nchini Morocco
mwaka huu. Katika taarifa iliyotumwa katika mtandao wake FIFA imedai kuwa
mfumo huo ulifanyiwa majaribio katika michuano ya Kombe la Shirikisho mapema
mwaka huu baada ya kampuni hiyo kushinda zabuni. Taarifa hiyo iliendelea
kudai kuwa kutokana na mafanikio yaliyopatikana katika majaribio ya mfumo huo
kwenye Kombe la Shirikisho FIFA inathibitisha kuwa GoalControl ndio watapewa
jukumu ya kufunga vyombo vinavyotumia mfumo huo kwenye michuano
hiyo. Mfumo wa GoalControl unatumia kamera 14 zenye uwezo wa hali ya juu
zinafungwa pembezoni kwa milingoti ya goli ili kuhakiki kama mpira umevuka
mstari au la.
TIKETI ZA KOMBE LA DUNIA 2014 KUPATIKANA KWA DROO YA BAHATI NASIBU.
SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA linatarajia kufanya
droo ya bahati nasibu kwa ajili ya tiketi za Michuano ya Kombe la Dunia baada
ya kupata maombi zaidi ya milioni sita ya tiketi hizo ikiwa ni mara mbili zaidi
ya tiketi zilizopo. Katika taarifa iliyotumwa katika mtandao wa FIFA
kumekuwa na jumla ya maombi 6,164,682 yametumwa kutoka nchi 203 huku zaidi ya
asilimia 70 ya maombi hayo yakitoka kwa wenyeji Brazil. Mechi ya ufunguzi
ya Brazil imepata maombi 726,067 na mechi ya fainali imepata maombi 751,165
huku kukiwa na nafasi ya tiketi 80,000 katika kila mechi. Mashabiki
wataruhusiwa tena kununua tiketi Desemba 8 baada ta kufanyika kwa droo ya
upangaji ratiba ambapo mechi ya ufunguzi inatarajiwa kupigwa jijini Sao Paulo
June 12 mwakani.
No comments:
Post a Comment