FERGUSON AMUONYA MOYES
MENEJA wa zamani wa klabu
ya Manchester United, Sir Alex Ferguson ametuma ujumbe wa onyo kwa mrithi wake
David Moyes kuwa siri kubwa ya mafanikio Old Traford ni umoja na maelewano
haswa katika vipindi vigumu. Kwasasa United inashika nafasi ya tisa katika
msimamo wa Ligi Kuu nchini Uingereza, ukiwa ni mwanzo mbaya zaidi kwa timu hiyo
katika miaka 20 iliyopita. Akizungumza katika semina na mafundisho ya ukocha
huandaliwa na Shirikisho la Soka barani Ulaya-UEFA, Ferguson amesema kuna vitu
vitatu vya msingi wakati unafanya kazi na benchi lako la ufundi ambavyo ni
maadili ya kazi, uaminifu na falsafa. Ferguson amesema ni muhimu watu wako
wakakubaliana na wewe na unavyotaka na njia unazotaka klabu yako icheze. Kocha
huyo aliendelea kudai kuwa ilikuwa ni vigumu zaidi kufanya kazi na watu miaka
30 iliyopita tofauti na sasa ambapo watu wengi aliokuwa nao walikuwa ni waelewa
na wanaotoka katika mazingira mazuri
No comments:
Post a Comment