Tuesday, October 15, 2013

MWANAMKE ASHITAKIWA KWA KUMNYONYESHA MTOTO WA JIRANI HUKU AKIWA NA VIRUSI VYA HIV


GABERONE, Botswana
MWANAMKE raia wa Zimbabwe aliyenyonyesha mtoto wa jirani bila ruhusa anakabiliwa na kifungo cha karibu miaka miwili kwa kumwambukiza mtu virusi vya HIV kimakusudi baada ya kupatikana na virusi hivyo.
Annie Mpariwa, 39, alifikishwa mbele ya mahakama ya Gaborone mnamo Jumatano na kesi hiyo kuahirishwa hadi Oktoba 24 kuruhusu kipimo cha pili cha HIV kufanyiwa mtoto huyo.
Matokeo ya kwanza ya mtoto huyo yalionyesha hana virusi ilhali mama huyo yalikuwa na virusi.
Mpariwa alikamatwa wiki jana kwa mashtaka ya usumbufu na iwapo mtoto huyo atapatikana na virusi mashtaka hayo yatazidishwa hadi 'kumwambukiza mtu mwingine HIV kimakusudi.
Mama ya mtoto huyo wa miezi 14, Nyasha Mironga, alisema kumwona mwanawe akinyonyeshwa na jirani wake ni jambo lilimshtua sana.
Kisa hicho kimetokea baada ya kupitishwa kwa sheria mpya ya HIV/Aids inayotoa adhabu kali zaidi kwa wale wanaowaambukiza wengine HIV kimakusudi.
Africa review.

No comments: