Saturday, October 19, 2013

MUME AUWAWA WAKATI HASUSI IKIENDELEA
Bi harusi mpya alilazimika kushuhudia mume wake mpya akipigwa risasi na kufa na wanaume wenye silaha walioficha sura zao kwenye sherehe ya harusi yao nchini Jamaica.
Jacqueline Cousins, miaka 49, aliolewa na Dameion Cousins, miaka 31, katika sherehe za kufana zilizofanyika huko Caribbean.
Lakini masaa kadhaa baadaye kundi lenye silaha likavamia kwnye sherehe hiyo wakidai Bwana harusi alikopa kwao Dola za Jamaica 10,000 - kiasi cha Pauni za Uingereza 60 tu.
Walimwelekezea Bi harusi mtutu wa bunduki wakati Dameion alipigwa risasi kichwani nje kwenye barabara.
Jacqueline, mfanyakazi wa kusaidia familia, kutoka Hornsey, North London, alisema hakuwa akifahamu kwanini genge hilo lilimlenga mume wake.
Alisema: "Nilianza kupiga mayowe na sikuweza kuamini kile nilichokuwa nakiona.
"Nililala chini kando yake na kuweka kichwa changu kifuani kwake. Nikagundua alikuwa amefariki.
"Tulikuwa watu wawili tu ambao tulipendana na nilipiga hatua hiyo kuwa pamoja na saa chache tu baadaye hili ndilo nililokuwa nikishughulika nalo."
Mama huyo wa watoto saba kwanza alikutana na Dameion - mwandishi wa nyimbo na mtumbuizaji - wakati alipotembelea nyumbani kwa wazazi wake nchini Jamaica miaka 11 iliyopita.
Wawili hao hawakuanza mahusiano hadi miaka saba baadaye wakati ndoa yake ya awali iliposambaratika.
Baada ya muda mrefu wa mapenzi ya mbali Dameion akamchumbia siku ya Mwaka Mpya 2012 na wawili hao wakaoana katika ndoa ya siri nyumbani kwake huko Hart Hill, Jamaica, Julai mwaka huu.
"Kulikuwa na zulia jekundu, na watu wapatao 17 tu pale tukiwamo sisi, sambamba na taa zinazomulika kwa mbali.
"Nilibeba maua kutoka kwenye bustani ya mama yangu na Dameion alitengeneza njia nzuri sambamba nao.
"Sikuwahi kumwona akiwa amefurahi kiasi kile."
Mke huyo mpya na mama mkewe wake Dorothy, miaka 80, walikuwa wakizungumza katika chumba cha ghorofani wakati majambazi wawili walipovamia ndani na kutaka kujua "wapi aliko Rasta?"
Walidai alikopa fedha taslimu kutoka kwao na mmoja wa wavamizi hao akaenda kutafuta vitu vya thamani.
Lakini wakati Dameion akivutwa kwenye barabara na wanawake hao wakasikia milio kadhaa ya risasi  kabla ya watu hao wenye silaha kutokomea.
Jacqueline aliyepagawa alimpata mumewe mpya akiwa amepigwa risasi kichwani na kwenye shingo.
Akikumbukia shambulio hilo, alisema: "Niliogopa sana kiasi cha kushindwa kuthubutu kuinua kichwa changu kuwatazama.
"Niliwaeleza hakuwapo pale, hivyo wachukue wanachotaka, lakini ilifanyika kwa haraka mno."
Polisi waliwakamata watu wawili kufuatia shambulio hilo baya, lakini wakawaachia bila kuwafungulia mashitaka na hakuna yeyote mwingine aliyekamatwa au kushitakiwa.
Wanandoa hao wapya walikuwa wamepanga kurejea London kumwezesha Jacqueline kuendea na kazi na mumewe mpya kuweza kupata kazi.
Jacqueline, ambaye alirejea Londo Agosti, alisema: "Ninachotaka ni majibu.
"Wanaume wawili ambao walimuua mume wangu bado wanaranda mitaani.
"Kila mtu alimpenda Dameion. Alipatana na kila mmoja. Nafikiri ilikuwa ni wivu kwamba ataiacha nchi hiyo na kuanza maisha mapya na mimi.

No comments: