TAARIFA MBALIMBALI KUTOKA TFF LEO
MECHI YA
YANGA, COASTAL YAINGIZA MIL 152/-
Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Yanga na Coastal Union iliyochezwa jana (Agosti 28 mwaka huu) katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 152,296,000. Watazamaji 26,137 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo namba 14 ya VPL msimu wa 2013/2014 iliyomalizika kwa sare ya bao 1-1. Viingilio katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 36,947,427.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 23,231,593.22. Mgawo mwingine ni asilimia 15 ya uwanja sh. 18,786,827.52, tiketi sh. 3,818,890, gharama za mechi sh. 11,272,096.51, Kamati ya Ligi sh. 11,272,096.51, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 5,636,048.26 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 4,383,593.09.

COPA
COCA-COLA KANDA KUANZA SEPT 2
Michuano ya
Copa Coca-Cola kwa vijana wenye umri chini ya miaka 15 inayoshirikisha mikoa
yote ya Tanzania Bara na Visiwani inaanza kutimua vumbi Septemba 2 mwaka huu
katika vituo sita tofauti. Kwa mujibu wa ratiba iliyopangwa leo (Agosti 29
mwaka huu), kituo cha Mwanza mechi zake zitachezwa katika viwanja vya Alliance
ambapo timu zitakazofungua dimba ni Kagera vs Kigoma, Mara vs Tabora, Simiyu vs
Geita na Mwanza vs Shinyanga. Kituo cha Mbeya ambapo mechi zitachezwa
viwanja vya Iyunga ni Katavi vs Njombe, na Ruvuma vs Mbeya. Kituo cha Pwani ni
Ilala vs Kaskazini Unguja, na Lindi vs Pwani. Ufunguzi katika kituo cha Arusha
ambapo mechi zake zitachezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta AMri Abeid
ni Manyara vs Kilimanjaro, na Arusha vs Singida. Uwanja wa Jamhuri ambapo
utatumika kwa mechi za kituo cha Morogoro, Tanga itacheza na Dodoma wakati
Morogoro itaumana na Temeke. Mjini Zanibar kwenye Uwanja wa Chuo cha Amaan ni
kati ya Kaskazini Pemba na Mjini Magharibi, na Kusini Pemba dhidi ya Kusini
Unguja.
USAILI WAGOMBEA TFF, TPL BOARD KUANZA KESHO
USAILI WAGOMBEA TFF, TPL BOARD KUANZA KESHO
Usaili kwa
wanaoomba kuteuliwa kuwa wagombea uongozi katika uchaguzi wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na ule wa Bodi wa Ligi Kuu (TPL Board) unaanza
kesho (Agosti 30 mwaka huu). Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Kamati ya
Uchaguzi ya TFF, Agosti 30 mwaka huu ni usaili kwa waombaji uongozi wote katika
Bodi ya Ligi Kuu pamoja na waombaji uongozi wa TFF kwa kanda namba 11 (Morogoro
na Pwani), kanda namba 12 (Kilimanjaro na Tanga) na kanda namba 13 (Dar es
Salaam). Agosti 31 mwaka huu ni kanda namba sita (Rukwa na Katavi), kanda
namba saba (Mbeya na Iringa), kanda namba nane (Njombe na Ruvuma), kanda namba
tisa (Lindi na Mtwara) na kanda namba kumi (Dodoma na Singida). Usaili kwa
kanda namba moja (Geita na Kagera), kanda namba mbili (Mara na Mwanza), kanda
namba tatu (Simiyu na Shinyanga), kanda namba nne (Arusha na Manyara) kanda
namba tano (Kigoma na Tabora), na nafasi za Rais na Makamu wa Rais wa TFF
utafanyika Septemba Mosi mwaka huu. Waombaji wote wamepangiwa muda wao wa
usaili. Kwa mujibu wa ratiba usaili ufanyika kuanzia saa 3 kamili asubuhi hadi
saa 2 usiku. Wasailiwa wote wanatakiwa kuzingatia muda waliopangiwa.
No comments:
Post a Comment