MKOA WA NJOMBE UNAONGOZA KWA TAKWIMU ZA UKIMWI NCHINI
TUME ya Kudhibiti UKIMWI nchini (TACAIDS) imesema mkoa wa Njombe unaongoza kwa kuwa na maambukizi makubwa ya Virusi vya UKIMWI kwa asilimia 14.8 ikifuatiwa na Iringa kwa asilimia 9.1.
Mkoa wa Mbeya unashika nafasi ya nne kwa asilimia tisa ukifuatiwa na
Ruvuma (7.2), Shinyanga (7.4), Dar es Salaam (6.9) Rukwa (6.2), Katavi (5.9),
Pwani (5.9),Tabora (5.1), Kagera (4.8) na Geita (4.7).
Msemaji wa TACAIDS, Glory Mziray alisema hayo jana Dar es Salaam na
wakati akizungumza na waandishi wa habari. Mikoa mingine na viwango vyake ni
Mara (4.5), Mwanza (4.2),Mtwara (4.10), Kilimanjaro (3.8), Kigoma (3.4), Simiyu
(3.6), Morogoro (3.8), Singida (3.3), Dodoma (2.9), Manyara (1.5), Lindi (2.9),
Tanga (2.4), Unguja (1.9) na Pemba (0.3).
Alisema takwimu hizo zinatokana na utafiti uliofanyika mwaka juzi hadi
mwaka jana. Kutokana na matokeo hayo, alisema maambukizi ya UKIMWI yamepungua
kwa kasi ndogo.
Alisema watanzania walioonesha kuwa na ufahamu sahihi wa elimu kuhusu
Virusi vya ukimwi na UKIMWI wanafikia asilimia 60 jambo linalosababisha kuwepo
mwamko mdogo wa kubadili tabia.
No comments:
Post a Comment