Tuesday, August 27, 2013

MAN UNITED NA CHELSEA HAKUNA MBABE
Cole akikabiliana na Rooney
Mourihno na Moyes wakipongezana
Mchezo wa ligi kuu nchini uingereza kati ya miamba wawili Man United na Chelsea usiku wa kuamkia leo umemalizika kwa sare ya bila kufungana kwenye Uwanja wa Old Trafford. 
Rooney alianza katika kikosi cha kwanza baada ya tetesi za muda mrefu majira haya ya joto kwamba atajiunga na Jose Mourinho Magharibi mwa London, lakini alipiga soka ya uhakika  akiwa na uzi mwekundu.
Chelsea ilianza bila washambuliaji wake Fernando Torres na Romelu Lukaku walioanzia benchi, lakini gumzo zaidi ni kila upande kulalamikia kunyimwa penalti katika mechi hiyo.
Katika mchezo huo wa kwanza wa Ligi Kuu ya Enlgand baina ya timu hizo, United ilianzisha washambuliaji watatu, Welebeck, Rooney na Van Persie. 
Dakika ya 65 Lampard alishika kabisa mpira kwenye eneo la hatari kufuatia shuti la Cleverley, lakini refa 'akapeta'.  
Dakika ya 71 Ashely Cole alianguka kwenye eneo la hatari wakati akikabiliana na Jones na akalilia penalti na hata Mournho akaonekana kulalamika akiwa kwenye benchi.  
Mchezo ulikuwa mkali na timu hizo zilishambuliana kwa zamu na baada ya mechi wachezaji walipongezana kwa mchezo mzuri.
Jose Mourinho alisema baada ya mechi mchezo ulikuwa wa haki na hadhani kama kuna iliyomzidi mwenzake uwezo, wakati Moyes alilalamikia penalti ya Lampard kuunawa mpira na kuwapongeza vijana wake kwa soka nzuri.

No comments: