Monday, July 1, 2013

BRAZIL YAUA SPAIN USIKU WA KUAMKIA LEO KOMBE LA MABARA


Fred akifunga bao la kwanza

Neymar akifunga bao la pili

David Luiz aliokoa kwenye mstari wa goli shuti la Pedro
Fred akishangilia bao lake la pili

Gerard Pique akionyeshwa kadi nyekundu baada ya kumfanyia madhambi Neymar aliyelala chini
Sergio Ramos akosa penalti
Wachezaji wa Brazili wakishangilia ushindi
David Luiz akiwa na mwali

BRAZIL, Usiku wa kuamkia leo walicheza Kandanda safi na kudhihirisha ‘JONGO BONITO’ ni kiboko ya ‘TIKI TAKA’ walipoisambaratisha Spain Bao 3-0 katika Fainali ya Kombe la Mabara iliyochezwa Estadio Do Maracana JijinI Rio De Janeiro Nchini Brazil.

Huku wakishangiliwa na Mashabiki wao Brazil, Mabingwa wa Dunia mara 5, waliwapiga Spain na kuwazidi kila hali kwa Bao za Fred, Bao mbili Dakika ya 2 & 47 na Supastaa Neymar Neymar 44na kumaliza Rekodi ya Spain ya kutofungwa katika Mechi 29 ya Mashindano rasmi.

Ulikuwa usiku wa balaa kwa Spain, ulimalizika kwa Sergio Ramos kukosa Penati Kipindi cha Pili na Gerard Pique kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu kwa kumuangusha Neymar yeye akiwa Mtu wa mwisho zikiwa zimesalia Dakika 22.

Mara baada ya Filimbi ya mwisho kulia, Mashabiki wa Brazil waliimba ‘MABINGWA WAMERUDI!’ huku Mitaa ya Rio De Janeiro ikifurika na Mashabiki waliokuwa wakicheza densi kwa furaha badala ya kuandamana kwa kahara kama walivyofanya kabla ya Mechi.

Nae Neymar alitwaa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Kombe la Mabara na kuzawadiwa Kiatu cha Dhahabu cha Adidas.

VIKOSI:

BRAZIL: Cesar; Alves, Silva, Luiz, Marcelo; Gustavo, Paulinho; Oscar, Fred, Neymar; Hulk

Akiba: Jefferson, Cavalieri, Fernando, Lucas, Hernanes, Dante, Luis, Jean, Rever, Bernard, Jo, Jadson.

SPAIN: Casillas; Arbeloa, Pique, Ramos, Alba; Xavi, Busquets, Iniesta; Mata, Torres, Pedro

Akiba: Valdes, Reina, Albiol, Martinez, Azpilicueta, Villa, Fabregas, Soldado, Monreal, Cazorla, Silva, Navas.

Refa: Bjorn Kuipers (Netherlands)

No comments: