TIMU YA MISRI YA KITAMA NDIYE MBABE WA DIWANI CUP NANYAMBA BAADA YA KUWAGAGADU WATANI WAO WA JADI KIROHO SAFI
 |
Sabasaba Stedium Nanyamba
|
 |
| Mgeni rasmi akikagua timu |
 |
| Kikosi cha Kiroho safi |
 |
| Kikosi cha Misri |
 |
| Mratibu Chanja boy akiwahasa manahodha na waamuzi |
 |
| Kamisaa wa mechi Alfred Mapunda |
 |
| Kabumbu imeanza |
 |
| Hekaheka langoni mwa Misri |
 |
| Kabumbu linaendelea ndani ya Sabasaba Stedium |
 |
| Mheshimiwa Diwani wa kata ya Nanyamba Hassani Mnauji kulia akiwa na Mgeni Rasmi Jeseph Tesha Kaimu afisa mtrendaji wa mamlaka ya maji mji mdogo Nanyamba wakifuatilia kabumbu kwa makini |
 |
| Nami sikuwa nyuma kuangalia kinachoendelea |
 |
| Ally Machemba Mkt wa kamati ya ligi ya Nanyamba akihakikisha mambo yanakwenda shwali |
 |
| Mashabiki |
 |
|

Usalama hawakuwa Nyuma kuhakikisha mambo yanakwenda sawa
Timu ya Misri ya Kitama kwa Wajanja jana imefuta uteja toka kwa watani wao wa jadi Kiroho Safi baada ya kuisambaratisha kwa mabao 2-1 katika mchezo wa fainali za Diwa Cup uliopigwa katika uwanja wa Sabasaba Nanyamba.
Mchezo huo ambao ulikuwa wa kuvutia karibu dakika zote, ulianza kwa timu ya Kiroho Safi wakilisakama lango la watani wao wa jadi mithili ya Simba aliye mawindoni na kusababisha kosa kosa nyingi langoni mwa Misri.
Iliwachukua dakika 27 Misri kupata bao la kuongoza kupitia mchezaji wao mashuhuri Hassani Zungu. Bao hilo liliamsha hasira kwa kiroho safi na kupeleka mashambulizi ya mara kwa mara kwa pasi fupifupi zenye uhakika lakini mashuti yao yaliokolewa na golikipa wa misri kwa umahiri mkubwa.
Hadi mapuziko Misri walikuwa mbele kwa bao 1-0.
Kipindi cha pili timu zilingia kwa lengo la kutafuta ushindi, lakini hali ilizidi kuwaendea vibaya Kiroho Safi pale Uwesu Uwesu alipoawainua mashabiki wa Misri katika dk ya 64 kwa bao safi lisilo na mushkeli.
Lakini kiroho safi walijitutumua na kupata bao la kufutia machozi kunako dk 72 kupitia Bushiri Nandala.
Hadi kipenga cha cha mwisho cha mwamuzi Hamisi Mastoka kinapulizwa mabao ni 2-1.
Katika fainali hizo mshindi wa kwanza alijinyakulia Tsh. 300,000 na mpira mmoja, mshindi wa pili 150,000 na mpira mmoja na mfungaji bora amepata sh.20,000.
No comments:
Post a Comment