HALI YA MTWARA MJINI KUANZIA JANA ASUBUHI MPAKA SASA NI TETE
![]() | ||||||||||
| Kamanda wa Polisi mkoani Mtwara Linus Sinzumwa |
Hali iivyokuwa jana asubuhi kabla ya vurugu
![]() |
| Stand kuu ya mabasi mjini mtwara jana asubuhi |
Hali baada ya vurugu
![]() |
| Magomeni |
![]() |
| Jengo la CCM Mtwara Vijijini |
Hali ya usalama ndani ya Mji wa Mtwara bado ni tete, inadaiwa baadhi ya watu
kupoteza maisha na wengine kadhaa
kujeruhiwa, milio ya mabomu ya machozi na bunduki kila kona bado vinaendelea
kulindima mapaka sasa.
Kwa mujibu wa kamanda wa Polisi mkoani Mtwara Linus Sinzumwa, Mtu mmoja amethibitishwa
kufa baada ya kupigwa risasi na polisi na majeruhi wanasizidi kuongezeka.Nyumba na baadhi ya ofisi za serikali zinadaiwa kuchomwa na moto.
Habari kutoka Mtaa wa Majengo zinadai kuwa vijana wamevamia ofisi ya CCM kata na ofisi ya serikali ya Kata hiyo na kuanza kuzibomoa, pia nyumba ya mwenyekiti wa CCM Manispaa ya Mtwara-Mikindani Ali Chinkawene imerushwa mawe.
Ofisi ya CCM Mtwara Vijini iliyopo eneo la Sabasaba nayo imechomwa moto na watu wasiojulikana.
Pia nyumba kadhaa za polisi na ya mtangazaji wa TBC Kasimu Mikongoro zimechomwa moto.
Katika mtaa wa Magomeni kundi la vijana linadaiwa kuwasha tairi la gari moto katikati ya barabara na huko Mikindani inadaiwa kuwa ofisi ndogo ya mbunge wa Mtwara Mjini, Asnein Murji nayo imechomwa moto.
Wanafunzi wa Shule za Msingi na sekondari walirejeshwa nyumbani mara baada ya mabomu ya machozi kuanza kurindima hewani hapo jana.
Tangu asubuhi ya jana kama ilivyokuwa Mei, 17 mwaka huu mji wa Mtwara ulikuwa kimya, huduma nyingi za kijamii zilifungwa, ukiwemo usafiri wa Pikipiki, Daladala, usafiri wa kwenda wilayani, Maduka, Soko kuu na kituo kikuu cha Mabasi.
Hali hiyo imejitokeza kufuatia kusambazwa kwa vipeperushi na watu wasiojulikana vikiwataka wafanyabishara mjini hapa kusitisha huduma za kijamii ili wasikilize Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini juu ya hatima ya madai yao ya kupinga mradi wa usafirishaji wa gesi kutoka Msimbati hadi jijini Dar es Salaam kwa njia ya bomba.
Hata hivyo wakazi wengi wamekosa fursa hiyo baada ya matangazo yanayorushwa na televisheni ya Taifa (TBC 1) kutopatikana kwa dishi za kawaida isipokuwa DSTV tangu juzi jioni, hata hivyo matangazo yalirejea jana muda mfupi baada ya Wizara ya Nishati na Madini kusoma bajeti yake.
Vipeperushi kama hivyo vilisambazwa mwanzoni mwa wiki iliyopita na kusababisha huduma za kijamii kusimama siku ya Ijumaa, Mei 17, 2013 vikidai kuwa siku hiyo bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini ingesomwa Bungeni hata hivyo haikusomwa.
Baadaye taarifa zilisema kuwa bejeti ya wizara hiyo ingesomwa Mei, 22 mwaka huu jana) hali iliyotoa nafasi kwa wandaaji wa vipeperushi hivyo kusambaza ujumbe mwingine wa kutaka huduma zisimame kwa siku ya jana na leo kwa njia ya simu za mkononi.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mtwara, Linus Sinzumwa ametaka wananchi kuendelea na shughuli zao kama kawaida lakini bado mpaka asubuhi ya leo hali si shwali kwani mabomu bado yanaendelea kulindima maeneo kadha ya mji wa Mtwara.
.jpg)






No comments:
Post a Comment