Thursday, May 2, 2013



 FAINALI YA WAJERUMANI WATUPU WEMBLEY LIGI YA MABINGWA BAADA YA BAYERN KUIKUNG'UTA 3-0 BARCA CAMP NOU NA KUFUZU KWA JUMLA YA 7-0
Bao la kwanza la Robben
Arjen Robben (katikati) akishangilia baada ya kufunga bao la kwanza
Sasa ndo umefanya nini, Kipa wa Barca, Victor Valdes akilalamika baada ya Pique kujifunga

Itakuwa fainali ya Wajerumani watupu Ligi ya Mabingwa Ulaya Uwanja wa Wembley wiki tatu zijazo Jumamosi, ikiwakutanisha Bayern Munich na Borussia Dortmund.
Hiyo inafuatia Barcelona kutandikwa mabao 3-0 nyumbani usiku wa leo, baada ya awali kuchapwa 4-0 Ujerumani, hivyo kutolewa kwa jumla ya mabao 7-0.
Barcelona walionekana kabisa kuzidiwa uwezo na mapema tu walionekana hawawezi kupanda mlima huo. Mabao ya Bayern ambao tayari ni mabingwa wa Ujerumani, wakiivua taji Dortmund, yamefungwa na Arjen Robben dakika ya 49, Gerard Pique aliyejifunga dakika ya 72 na Thomas Muller dakika ya 7.

No comments: