Sunday, April 7, 2013

LULU NA MAMA KANUMBA WAONGOZA MAELFU KUWEKA SHADA KWENYE KUMBUKUMBU YA KANUMBA LEO

Mama Kanumba na Lulu wakiwa wamekumbatiana baada ya misa maalum ya kumuombea marehemu Kanumba


Baadhi wa wadau wa Tathnia ya filamu wakiweka mashada ya maua kwenye kaburi la marehemu Steven Kanumba 


Wapenzi wa filamu za kitanzania walioko jijini dar es salaam, leo hii walipata fursa ya kuungana na wasanii mbalimbali wa filamu nchini katika kuadhimisha kumbukumbu ya mwaka mmoja toka kufariki kwa msanii nguli wa filamu nchini Steven Kanumba ambaye alifariki tarehe kama ya leo mwaka mmoja uliopita.

Tukio hilo lilihudhuriwa na watu kibao ambapo pamoja na mambo mengine, watu mbalimbali walipata fursa ya kuweka mashada ya maua kwenye kaburi la marehemu, wakiongozwa na mama mzazi wa msanii huyo pamoja na binti Elizabeth Michael “Lulu”, ambaye anakabiliwa na tuhuma za kushiriki katika kifo cha msanii huyo.

Picha kwa hisani ya pallangyor.blogspot


No comments: