CITY YAUA UTD NYUMBANI KWAKE.
![]() |
| Mkali Aguero |
![]() |
| Mshike shike |
Kama unakumbukumbu nzuri Aguero ndiye bao lake liliipa ubingwa wa Ligi Kuu Manchester City msimu uliopita na usiku wa leo ameifungia timu hiyo bao la ushindi zikiwa zimesalia dakika 11 mchezo kwisha Uwanja wa Old Trafford na kuipa ushindi mfululizo timu hiyo dhidi ya wapinzani wao hao kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 41.
Kipigo hicho cha kwanza kwa United tangu Novemba, pia kimemaliza rekodi yao ya kutofungwa ndani ya mechi 18 na kupunguza idadi ya pointi zao za kuongoza kileleni mwa Ligi Kuu hadi kubaki 12.
Zikiwa zimesalia mechi saba tu Ligi Kuu kufikia tamati, bado United wana nafasi kubwa ya kutwaa uibingwa.
James Milner alitangulia kuifungia Man City dakika ya 51, lakini Nahodha Vincent Kompany akajifunga kuisawazishia United dakika ya 59 kabla ya Aguero kufunga la ushindi dakika ya 78.
Katika mchezo huo, kikosi cha Manchester United kilikuwa: De Gea, Rafael, Evra, Jones, Ferdinand, Giggs, Carrick, Young/Kagawa dk90, Rooney/Hernandez dk85, Welbeck/Valencia dk80 na Van Persie
Manchester City: Hart, Zabaleta, Kompany, Clichy, Nastasic, Milner, Nasri/Aguero dk71, Barry, Silva/Lescott dk90, Y Toure na Tevez/Garcia dk90.



No comments:
Post a Comment