BWAWA LA MAJI LA CHIPITE MTWARA LA PUNGUA
Hali ya bwawa la chipite wananchi na magari wakivuka na mizigo |
Baada ya Maji kupungua katika eneo la Chipite ambalo lilijaa maji na kusababisha Abiria zaidi ya 500 na Magari zaidi ya 200 kushindwa kupita eneo na Kufanya gari nyingi ziendazo na Kutoka Mtwara,Masasi,Ruangwa,Liwale,Nachingwea,Liwale,Nanyumbu na Tunduru kufanya safari kwa kuzunguka wilaya ya Newala sasa hali imeanza kubadilika na gari nyingi kuanzia jioni zimeanza kupita ingawa kwa
Mashakamashaka ili kusaidia kupeleka na kutoa huduma kwa Jamii
Kufuatia hali hiyo baadhi ya wasafiri waliokwama wametupia lawama kwa Wakala wa Barabara Tanroads na Kitengo cha Maafa kutotoa Ushiriakiano wowote kuhakikisha Abiria wanakuwa kwa usalama ikiwa pamoja na kutafuta jitihada za haraka kuwavusha ili kuepusha Maafa yatakayochangiwa na uwepo wa msongamano kwa muda mrefu Hali ya usafiri sasa iko kama kawaida kuelekea katika wilaya Tajwa hapo juu.
Na Abdulaziz Lindi
No comments:
Post a Comment