Saturday, March 9, 2013

YANGA YAZIDI KUCHANJA MBUGA LIGI KUU YAUA TOTO, AZAM YAKWAMA CHAMAZI



BAO pekee la kiungo Nizar Khalfan leo, limezidi kuipaisha Yanga SC kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Toto Africans Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kwa ushindi huo, Yanga imefikisha pointi 45 baada ya kucheza mechi 20 hivyo kuzidi kujitanua kileleni mwa Ligi Kuu kwa pointi nane zaidi, dhidi ya Azam FC wanaoshika nafasi ya pili, wakati kwa Toto imezidi kujichimbia kaburi.

Katika mechi hiyo iliyochezeshwa na refa Andrew Shamba, aliyesaidiwa na Abdallah Mkomwa na Abdallah Rashid, hadi mapumziko ngoma ilikuwa ngumu.

Yanga WALIPATA bao katika dakika ya 78, krosi maridadi ya Hamisi Kiiza iliunganishwa nyavuni na Nizar.

Katika mechi nyingine ya ligi hiyo, Azam FC ilitoka sare ya 1-1 na Polisi Morogoro kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam, hivyo kufikisha pointi 37.

John Raphael Bocco alitangulia kuifungia Azam FC dakika ya nne na Mokili Rambo akaisawazishia Polisi kwa penalti dakika ya 55.

Kesho simba na coast uwanja wa Tifa DSM

No comments: