SOPHIA SIMBA AHAIDI KUKABILI UNYANYASAJI DHIDI WA WANAWAKE
Na Mwandishi Maalum
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Sophia Simba ( Mb) amesisitiza kwamba, serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua wazi kwamba unyanyasaji dhidi ya wanawake na watoto wa kike ni ukiukwaji wa haki za binadamu na kwamba vitendo hivyo vina madhara makubwa.
Kwa kulitambua hilo, Waziri anasema serikali zote mbili ile ya Tanzania Bara na Visiwani, zimekuwa zikichukua hatua pamoja na kutekeleza mikakati mbalimbali ya kuhakikisha kwamba unyanyasaji dhidi ya kundi hilo la jamii wakiwamo watu wenye ulemavu wa ngozi ( albino) unapunguzwa na hatimaye kutokomezwa.
Waziri ameyasema hayo jana alhamisi, wakati alipokuwa akitoa mchango wake wakati wa majadiliano yaliyohusu ajenda ya utokomezaji na upunguzaji unyanyasaji dhidi ya wanawake na watoto wa kike.
Mhe.Sophia Simba anaongoza ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano wa 57 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya wanawake ( CSW), ambao umeanza siku ya jumatatu hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, New York , Marekani.
Amezitaja hatua hizo kuwa ni pamoja na tatizo la unyanyasaji kuainishwa katika Mpango wa Kitaifa wa Kupunguza Umaskini ambapo vitendo hivyo vinaelezwa kama kiashiria cha umaskini.
Aidha akaeleza pia kwamba mipango mbalimbali ya utekelezaji katika ngazi ya kitaifa na kwa kushirikiana na sekta mtambuka imeundwa kwa pande zote mbili za Muungano.
Vile vile akabainisha kwamba, taasisi za kisheria kama vile Chama cha Majaji wanawake, zimekuwa zikitoa mchango mkubwa katika kuwasaidia wanawake fursa ya kupata haki.
Kama hiyo haitoshi, Waziri Sophia Simba amesema, kwa upande wa vyombo vya ulinzi na usalama kumeanzishwa pia mtandao wa Polisi wanawake lengo likiwa ni kuwawezesha na kuwapa nyenzo za kushughulikia kikamilifu matukio ya unyanyasaji wa kijinsia.
Pamoja na juhudi mbalimbali zinazofanywa na serikali na wadau wengine, Waziri Sophia Simba hakusita pia kubainisha baadhi ya changamoto zinazokwamisha juhudi hizo.
Amezitaja baadhi ya changamoto kuwa ni pamoja kutokuwapo kwa takwimu za uhakika kuhusu vitendo vya unyanyasaji, takwimu ambazo zingeweza kuchangia katika uaandaaji wa sera na mipango mbalimbali yenye kulenga kusukuma maendeleo ya wanawake.
Akataja changamoto nyingine kuwa ni ile ya kubadili mtizamo wa jamii kuhusu suala zima la unyanyasaji wa jinsia na kwamba tatizo hilo linahitaji kuendelea kufanyiwa kazi.

No comments:
Post a Comment