MKE AMUUWA MUMEWE KWA KISU KWA WIVU WA MAPENZI.
![]() |
Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro Robert Boaz |
MWANAMKE mmoja aliyefahamika kwa jina la
Happyness Mrema (28) amemchoma kisu mumewe Audiphas Mrema (30) na kumuuwa
kutokana na ugomvi wa wivu wa mapenzi. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini
kwake, Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro Robert Boaz, alisema tukio hilo
lilitokea Machi 9, 2013 katika Kijiji cha Kikelelwa wilayani Rombo mkoani
Kilimanjaro, ambapo mwanamke huyo alimchoma kisu mumewe na kumsababishia mauti
papohapo.
Kwa mujibu wa Kamanda Boaz, siku ya tukio marehemu alifika nyumbani saa moja
usiku na kumkuta mkewe amenuna ndipo ulipozuka ugomvi. “Inadaiwa kuwa baada ya
mume huyo kuja saa moja mke alimuhoji kwa nini amechelewa kurudi ndipo ugomvi
ulipoanza ambao unaelezewa ni wivu wakimapenzi na hatimaye mke kumchoma kisu mumewe na kufa papohapo,” alisema.
Aidha kamanda alisema mwanamke huyo anashikiliwa na polisi na kwamba atafikishwa mahakamani wakati wowote uchunguzi utakapokamilika.
No comments:
Post a Comment