ALIYEMUUA MGONI WAKE NAYE AUAWA
![]() |
Kijana Peter Bosco baada ya kupigwa na na wananchi wenyae hasira kali |
KIJANA Peter Bosco mkazi wa Itiji, mjini Mbeya aliyedaiwa
kumuua kwa kumchoma kisu kifuani mgoni wake Daniel Mwasalemba Februari 8, mwaka
huu, naye amefariki dunia baada ya kupigwa kwa mawe na watu wenye hasira kali.
Kwa mujibu wa ndugu wa Peter, marehemu alifariki baada ya
kupata majeraha kadhaa siku anayodaiwa kuua kutokana na kupigwa kwa mawe na
watu hao.
“Watu wenye hasira kali walimpiga kwa mawe Peter siku ya tukio na kusababisha polisi wampeleke hospitali alikolazwa baada ya kuumia, amefariki hivi karibuni na tayari ameshazikwa,” alisema ndugu huyo.
Peter anadaiwa kumuua Daniel kwa kumchoma kisu kifuani na kumburuta marehemu hadi kando ya barabara huku akiwa uchi wa mnyama baada ya kumfumania na mwanamke wake aitwaye Elizabeth Michael.

Elizabeth ambaye ni maarufu kwa jina la Lulu wa Mbeya
ambaye kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, ACP Diwani Athmani, ni
muuza pombe za kienyeji katika klabu iitwayo Musoma iliyopo Itiji, Mbeya.
Kamanda Diwani alisema chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa kimapenzi baada ya Peter kumfuma Daniel akiwa nyumbani kwa mwanamke huyo ambapo aliwafungia mlango kwa nje na kwenda kutafuta kisu alichokitumia kumuua mwenzake.

Source: Globpublishers.
No comments:
Post a Comment