Saturday, March 9, 2013


MALKIA WA NYUKI AKUTANA NA TAWI LA MPIRA PESA
Rahma Al Kharoos
Malkia wa nyuki usiku wa kuamkia leo amefika kwennye tawi la mpira pesa lililoko Magomeni Mikumi kwa ajili ya kutafuta suhulu ya mgogoro uliopo kati yao na uongozi wa Simba.

Malkia wa nyuki kwenye kikao hicho alikuwa ameambatana na wajumbe wa kamati ya utendaji ya Simba na wanachama wa tawi hilo walimpa masharti kadhaa baada ya kukaa kikao kilichochukua takribani saa tatu.

Moja ya masharti aliyopewa ni kuwa uongozi wa Simba ulilifuta tawi hilo kwa kuwapa barua na kutangaza kwenye vyombo vya habari hivyo wanataka taratibu zilizotumika kulifuta zitumike kulirudisha tena.

Pili wametaka uitishwe mkutano Marchi 17 kwa ajili ya kutafuta mstakabali wa klabu ya Simba katika kufanikisha kumalizia michezo nane ya ligi kuu iliyobakia.

Tatu tawi hilo linamtaka Mwenyekiti Ismail Rage na yeye ajiuzulu kama walivyofanya akina Kaburu.

Kikao hicho kilifanyika kwa utulivu na kukubaliana kamati ya utendaji ya Simba inakwenda kukaa na kuyafanyia kazi ili wajenge Simba upya. 

pallagyor.blogspot.com

No comments: