NDOA YA MIAKA MINNE YAVUNJIKA KWA SABABU YA UDOGO WA UUME
Mwanamke huyo aliyetajwa kwa jina la Zhang mwenye umri wa miaka 52, amevunja ndoa yake ya miaka minne na mumewe Zhou mwenye umri wa miaka 55 sababu kubwa ikiwa ni udogo wa uume wake.
"Uume wake ni mdogo sana sawa na wa mtoto, una urefu wa sentimita tano tu, hatujawahi kufurahia mapenzi kwa muda wote wa ndoa yetu", alisema Zhnag.
Zhang aliongeza kuwa alikutana na mumewe mwaka 2008 kupitia kwa rafiki yake na walifunga ndoa miezi mitano baadae.
Zhang aliendelea kusema kuwa kabla ya ndoa hawakuwahi kufanya mapenzi kwakuwa mumewe huyo alikuwa akidai kuwa yeye ni mtu wa dini sana hawezi kufanya mapenzi nje ya ndoa.
"Niligundua tatizo alilonalo siku ya harusi", alisema Zhang na kuongeza "Pia hajiwezi kutimiza majukumu yake ya kutoa unyumba kwa mkewe".
"Tuligombana usiku mzima na nilimwambia afanye hima kutafuta tiba" alisema Zhang ambaye sasa amefanikiwa kuivunja ndoa hiyo kupitia mahakama.
Hii sio mara ya kwanza kesi za kuvunja ndoa kufika mahakamani sababu ikiwa ni ufanisi kwenye tendo la ndoa.
Mwaka 2008, Mwanaume mmoja wa nchini Urusi alikimbiwa na mkewe baada ya kwenda kufanya operesheni ya kuongeza ukubwa wa uume wake lakini wakati wa malavidavi kipande kilichoongezwa kwenye uume kilinyofoka.
No comments:
Post a Comment