Saturday, March 23, 2013

AMA KWELI MAPENZI NI KIZUNGUMKUTI

KIJANA AWA GUMZO DUNIANI BAADA YA KUANDAA VIDEO YA KUOMBA MSAMAHA HUKU AKILIA.

Kijana mmoja wa nchini Marekani amekuwa gumzo duniani baada ya kuandaa video akilia kusamehewa na mpenzi wake lakini mpenzi wake huyo akaamua kuianika kwenye internet video hiyo na kumfanya mwanaume huyo awe kituko.
” Bebi nisamehe, unajua jinsi gani ninavyopata tabu, kwanini umeondoka na kuniacha hivi", alianza kuongea kijana huyo akililia penzi la mpenzi wake wa zamani ambaye ameamua kumkimbia.

Kijana huyo alitengeneza video kuonyesha uchungu wake kwa kuachana na mpenzi wake huyo na kumpelekea video hiyo aiangalie labda akiona machozi yake atamsamehe na kumrudia.

"Nakupenda sana, najua watu wananiambia nastahili mwanamke bora zaidi yako lakini simtaki mwingine yeyote nakutaka wewe tu, tafadhali tafadhali bebi", aliendelea kumwaga chozi kijana huyo akigeuza kofia yake mbele nyuma.

Mpenzi wa kijana huyo badala ya kutoa msamaha aliamua kuianika video hiyo kwenye YouTube na kupelekea mwanaume huyo kuwa kituko watu wakitoa maoni mbalimbali.

Baadhi ya watu walimuonea huruma na kumlaani mpenzi wake kwa kuzianika hisia za mpenzi wake kwenye internet.

Watu wengine walitoa maoni wakimtaka kijana huyo asimame kama mwanaume na aache kulialia kama mwanamke.


Angalia VIDEO ya kijana huyo chini


No comments: