MTOTO WA MIAKA 8 ALIYEOA BIBI WA MAIAKA 61 ADAI SASA ANAJISIKIA FURAHA KUITWA BABA
KUSHOTO: Sanele akibusiana na mkewe, Helen siku ya harusi yao wiki mbili zilizopita. KULIA: Sanele na Helen walipata chakula cha usiku pamoja nyumbani kwa mkewehuyo
Mtoto, Sanele Masilela, mwenye miaka 8, anafurahia chakula cha usiku na mke wake, baada ya kumuoa wiki mbili zilizopita, na inasemekana kwa sasa ameanza kujisikia kama mume kamili.
Mwanafunzi huyo alimuoa Helen Shabangu baada ya mizimu kumweleza kwamba anatakiwa kuoa.Mwanafunzi huyo alimchagua rafiki wa familia yao na mama wa watoto watano Helen na familia yake ikalipa Pauni za Uingereza 500 kuwezesha mama huyo kuwa mkewe katika sherehe iliyogharimu Pauni 1,000 mjini Tshwane, Afrika Kusini.
Sanele alikiri kwamba tangu harusi hiyo, ameanza kujisikia kama mwanandoa.Alisema: "Siku hiyo ilikuwa ya kipekee na hakika ilikuwa kama alivyokuwa akifikiria itakuwa."Marafiki zangu walifikiri ni mzaha kwamba nilikuwa naoa lakini sasa najisikia kama mume."
Akiwa amevalia tai na suti ya rangi ya shaba, Sanele, mtoto wa mwisho katika familia ya watoto watano, alivalishana pete mbele ya wageni 100 na hata kufikia kupigana mabusu na mkewe huyo.Lakini, licha ya muonekano, haikuwa halisia, ndoa hiyo ilikuwa ni kutimia mila na haikufungwa kisheria.Wanandoa hao hawaishi pamoja lakini Helen mara kwa mara anamwalika kula naye chakula cha usiku pamoja kwenye nyumba anayoishi na familia watoto wake.Sanele amerejea kwenye maisha yake na kuendelea kufurahia shule na kucheza kandanda na marafiki zake lakini anakiri kwamba ndoa hiyo ilikuwa muhimu mno kwake.Habari za harusi hiyo zimeshitua dunia nzima lakini Helen, ambaye ameshaolewa kwa miaka 30 sasa na kupata watoto watano wenye umri wa kati ya miaka 37 na 27, ametetea sherehe hiyo.Alisema: "Nafahamu habari hiyo imesambaa dunia nzima na kubwa ni kuwa nchi nyingine zimeweza kujifunza kuhusu utamaduni wetu na mababu zetu.Helen alikiri sherehe hiyo ya gharama ilikuwa kubwa kuzidi ilivyokuwa harusi yake halisi na mumewe, Alfred, mwenye miaka 65, na hakuna cha kujutia. Mama wa Sanele mwenye miaka 46, Patience Masilela aliongeza kwamba anaamini sherehe hiyo 'haikuwa na tatizo' na kwamba imewatuliza mababu.Alisema: "Hii ni mara ya kwanza kutokea katika familia hiyo.
No comments:
Post a Comment