LIGI kuu nchini
Uingereza inatarajiwa kuanza kutumia mfumo wa teknologia ya kompyuta
katika mstari wa goli wakati msimu mpya wa ligi hiyo 2013-2014. Mfumo
huo ulifanyiwa majaribio na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA katika
michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia iliyofanyika Desemba mwaka jana na
tayari viongozi wa ligi hiyo wameshaanza mazungumzo na kampuni
zilizopewa dhamana ya kufunga vifaa hivyo.
Msemaji
wa ligi hiyo Dan Johnson amesema mara msimu ujao utakapoanza klabu zote
zitalazimika kuwa na mfumo huo zikiwemo klabu ambazo zitakuwa zimepanda
daraja.
Mifumo
miwili ya Hawkeye na GoalRef ambayo ndio imepitishwa na FIFA yote
ilitumika katika michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia kwa mafanikio.
No comments:
Post a Comment