MSHAMBULIAJI wa
kimataifa wa Ivory Coast, Didier Drogba ameruhusiwa kuendelea kuichezea
klabu ya Galatasaray katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya
Shirikisho la Soka la bara hilo-UEFA kutupilia mbali madai ya klabu ya
Schalke 04 ya Ujerumani. Drogba
mwenye umri wa miaka 34 alicheza mchezo wake wa kwanza akiwa na
Galatasaray katika michuano hiyo ya Ulaya dhidi ya Schalke Februari 20
katika hatua ya timu 16 bora ambao ulimalizika kwa sare ya bao 1-1. Baada
ya mchezo huo klabu ya Schalke ilipeleka malalamiko yake UEFA ikidai
kuwa nyota huyo wa zamani wa UEFA hakusajiliwa kwa wakati ambao
ungemuwezesha kucheza mechi za michuano hiyo. Hata
hivyo UEFA ilitupilia mbali madai hayo ambapo kama Galatasaray
wangekutwa na hatia ya kuchezesha mchezaji huyo kinyume cha sheria
Schalke wangepewa ushindi wa mabao 3-0. Drogba amesajiliwa na Galatasaray kwa mkataba wa miezi 18 akitokea klabu ya Shanghai Shenhua ya China.
No comments:
Post a Comment