Saturday, February 9, 2013

WAZIRI MKUU WA SERBIA KIJASHO CHEMBAMBA CHAMTOKA BAADA YA MTANGAZAJI WA TV KUVAA NUSU UCHI WAKATI WA MAHOJIANO


Waziri Mkuu wa Serbia akiwa katika mahojiano

Kijasho chembamba kilimtoka Waziri Mkuu wa Serbia, ambaye pia aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Ivica Dhati, pale alipoalikwa kwenye kipindi cha televisheni na kufanyiwa manjonjo ya kila namna na mtangazaji mrembo aliyekuwa amevaa nusu uchi.

Waziri Mkuu huyo alikumbwa na wakati mgumu, hakujua afanye nini wakati mtangazaji mmoja mrembo wa nchini Serbia alipokuwa akimfanyia mahojiano waziri huyo akiwa amevaa nusu uchi huku akiwa hana nguo ya ndani.

Awali Waziri Mkuu huyo alifika katika Jengo la kituo hicho cha televisheni kwa kushiriki kipindi cha mahojiano, bila ya kujua kwamba atashiriki katika kipindi cha Mission Impossible, ambacho hurushwa katika kituo cha pink.

Kipindi hicho kilianza huku kukiwa na kamera zilizokuwa zimefichwa zikirikodi mahojiano hayo, wakati huo mtangazaji wa kipindi hicho alikuwa amevaa nguo fupi huku akiwa hana nguo ya ndani.

Tukio ambalo limethibitishwa na Mshauri Maalum wa usalama wa taifa wa nchi hiyo Ivica Tonstev, ambaye alielezea tukio hilo kama ni la kijinga limeifedhehesha Serbia na si Waziri Mkuu.

Sehemu ya Video hio yenye utata ya kipindi hicho imejipatia umaarufu mkubwa katika mtandao wa "YouTube", kiasi cha kutazamwa na watu milioni 1.7 chini ya masaa 48, kwa mujibu wa shirika la "Rianovosty".

No comments: